IQNA

Hija 1445

Usajili wa Hija 1445 Hijria wafunguliwa Saudi Arabia

15:27 - February 13, 2024
Habari ID: 3478344
IQNA - Usajili umefunguliwa kwa raia wa Saudi au wakaazi nchini walio tayari kushiriki katika ibada ya Hija ya mwaka 1445 Hijria/ 2024.

Wizara ya Hijja na Umrah ya Saudi ilitangaza ufunguzi wa usajili siku ya Jumapili.

Wale wanaotaka kuhiji kutoka kwa Ufalme wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti ya wizara localhaj.haj.gov.sa au kupitia programu ya Nusuk kwenye simu  ya mkononi au kompyuta kuanzia saa moja jioni Jumapili, Februari 11.

Huko wanaweza kukagua chaguo vifurishi mbali mbali vya Hija, huku uhifadhi ukipewa kipaumbele kwa wale ambao hawajawahi kuhiji hapo awali.

Ili kurahisisha usajili, wizara imewezesha ama kulipa kiasi chote baada ya usajili au kulipa kiasi fulani kulingana na sheria na masharti yaliyotajwa.

Wizara iliwataka waliojiandikisha kuhakikisha usahihi wa taarifa wakati wa kusajili na kuchagua vifurushi, ikisisitiza umuhimu wa kutotumia nambari moja ya simu kwa zaidi ya programu moja.

Maswali yanaweza kutumwa kwa wizara kupitia barua pepe kwa care@haj.gov.sa, kwa kupiga simu kwa Kituo cha Huduma ya Mahujaji  kupitia 1966 kutoka ndani ya Ufalme au kupiga nambari 920002814 - kutoka ndani na nje ya Ufalme, au kupitia kwenye X: @MOHU_Care.

Hija ni safari ya kwenda Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na uwezo wa kifedha analazimika kuitimiza angalau mara moja katika maisha yake.

Takriban Waislamu milioni 2.5 kutoka sehemu mbalimbali za dunia hushiriki katika ibada ya Hija kila mwaka.

3487160

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija saudi arabia
captcha