IQNA

Ajali

Watu 20 wapoteza maisha katika ajali ya Basi wakiwa safari ya Umrah Saudi Arabia

14:23 - March 28, 2023
Habari ID: 3476774
TEHRAN (IQNA) – Takriban waumini 20 waliokuwa katika hija ndogo ya Umrah wamepoteza Maisha na wengine 29 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa limewabeba lilipopinduka na kuwaka moto katika eneo la Aqaba Shaar kusini mwa mkoa wa Asir, Saudi Arabia Jumatatu alasiri.

Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Aqaba Shaar inayounganisha mji wa Abha na mkoa wa Mahayil Asir.

Basi la abiria lilipoteza mwelekeo kufuatia kufeli breki na kugonga daraja na kupinduka na kuwaka moto. Wasafiri walikuwa wakielekea Makka kufanya Umra.

Vikosi vya Ulinzi wa Raia na Hilali Nyekundu ya Saudia pamoja na mamlaka za usalama walikimbilia eneo la tukio baada ya kupata taarifa kuhusu ajali hiyo na kuanza shughuli za uokoaji.

Mwendo wa trafiki ulitatizwa kando ya barabara kwa saa kadhaa kufuatia ajali hiyo. Miili ya waliopoteza Maisha na majeruhi imepelekwa katika hospitali kadhaa mkoani humo.

3482964

Kishikizo: umrah saudi arabia
captcha