IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/33

Kazi ya Kuchambua Misahafu ya Hati ya Zamani

20:54 - December 03, 2023
Habari ID: 3477982
TEHRAN (IQNA) – Kitabu cha “Nakala za Qur'ani (Misahafu) za Bani Umayya: Muhtasari wa Kwanza” cha mwanazuoni mashuhuri wa Kifaransa Francois Deroche ni mojawapo ya vitabu muhimu vya kisasa vya hati za Qur’ani.

Kazi hii  kuu ya kitaaluma inachambua nakala za kwanza za Qur'ani Tukufu.

Francois Deroche (alizaliwa Oktoba 24, 1952) na ni msomi na mtaalamu wa Codicologia na Palaeografia. Yeye ni profesa katika Chuo cha Collège de France, ambako ni Mwenyekiti wa "Historia ya Maandishi ya Qur'ani na Usambazaji".

Katika mahojiano na jumuiya ya watafiti wa Qur'ani IQSA, Dk Deroche amezungumzia suala la maandishi au hatu za Qur'ani katika zama za Umayyad.

Alidai katika mahojiano haya kwamba Misahafu ya zama hizo imekuwa na taathira katika kuenea kwa qiraa ya Qur'ani na kwamba hati za Misahafu ya muongo wa kwanza wa utawala wa Bani Umayya zilikuwa dhaifu.

Alisema alikuwa amepanga kufanya utafiti zaidi kuhusu Misahafu ya zama za Bani Umayya kwa mapana zaidi, na kuongeza kuwa nyenzo zilizotumika katika zama hizo hazikurekodiwa na hazina historia. Ndiyo maana alianza kwa kufanyia kazi historia ya hati za zaidi ya miongo mitatu za zama za utawala wa Bani Umayya. Hilo lilipelekea kuangaliwa kwake upya kwa maoni yake ya awali juu ya maandishi ya Qur'ani, kwa mfano, haja ya kuangalia kwa uangalifu zaidi tarehe ya Misahafu ya kale.

Deroche alisema Kitabu cha “Nakala za Qur'ani (Misahafu) za Bani Umayya: Muhtasari wa Kwanza” sio tu kinatoa historia ya maandishi ya zama hizo bali pia kinaonyesha kwamba maendeleo ya aina ya uandishi, hasa sheria za tahajia, yalikuwa ya haraka.

Alisema kitabu hicho kinatanguliza vipengele vipya vya historia ya uandishi wa Kiarabu na kinaonyesha kuwa historia ni suala muhimu katika kusoma yaliyojiri  zama hizo.

Kitabu hicho kilileta vipengele vipya kwenye historia ya sanaa ya Kiislamu katika zama hizo na kutoa mtazamo mpana zaidi kuhusiana na suala hili, alisema.

Faida ya kwanza ya kitabu hiki ni kwamba kwacho mtu anaweza kuzungumzia sanaa katika zama za Bani Umayya, na pia kinatoa mtazamo mpya kuhusu maoni ya watawala wa juu kuhusu Quran, alisema.

Deroche anatamani angeweza kuleta ushahidi wa kusadikisha wa kuhusishwa na baadhi ya maandishi ya enzi ya Bani Umayya. Anasisitiza kwamba sura ya mwisho ya kitabu chake inaweza kuwa mwanzo wa kwenda nje ya zama za Bani Umayya na kusoma maandishi ya zama za Bani Abbas, ambayo hakuna utafiti mwingi umefanywa.

Hivi sasa, anafanyia kazi nakala ya Kiarabu ya Misahafu ya  Bani Umayya kama sehemu ya kwanza ya mradi wa utafiti. Kitabu kina maneno mengi yenye tafsiri tofauti.

Baadhi ya wasomi wanaamini kwamba Deroche katika utafiti wake kuhusu Misahafu  amekuwa na mtazamo wa kilimwengu, akifanya utafiti wake kama Mfaransa Mtaalamu wa Masuala ya Mashariki. Hata hivyo, wanasema kitabu chake kina faida mbili. Kwanza, kinakanusha madai yaliyotolewa na baadhi ya Mustashrikin (wasomi wa Magharibi ambao ni wataalamu wa masuala ya Mashariki)  wanadai kwamba eti Qur'ani Tukufu iliandikwa kikamilifu karne ya 4 Hijri, na pili, kitabu hicho kinatuhimiza kusoma nakala za zamani za Qur'ani ambazo idadi kubwa zipo. Moja Msahafu ambao Deroche amechunguza unajulikana kama nakala ya Parisiano. Ilipatikana katika Msikiti wa Amr ibn al-Aas huko Cairo na ilipelekwa kwenye Bibliothèque nationale de France (maktaba ya kitaifa) huko Paris katika karne ya 19 Miladia.

Habari zinazohusiana
captcha