Msahafu huo wa kihistoria ulioandikwa kwa mkono na Seyyid Süleyman Vehbi Efendi katika karne ya 19, umekabidhiwa msikiti huo hivi karibuni.
Mustafa Usser, makamu wa rais wa bodi ya wakurugenzi wa msikiti huo, alionyesha furaha yake ambapo amesema: "Jamii yetu imepewa nakla ya Qur'ani ya kihistoria kutoka karne ya 19, iliyoandikwa kwa mkono na Seyyid Süleyman Vehbi Efendi. Kazi hii ya thamani, inayokadiriwa kuwa iliandikwa kwa mkono kati ya 1860 na 1872 Miladia, itaimarisha sana urithi wetu wa kiroho na kiutamaduni. Tunafurahia kupokea zawadi isiyosahaulika kama hii."
Usser amebaini kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ilitolewa na Dk. Elke Niewöhner, mwanafunzi wa masomo ya Kiislamu, ambaye alipata maandishi hayo kutoka kwa Jens Kröger, mtunzaji wa zamani katika Jumba la Makumbusho ya Sanaa ya Kiislamu ya Berlin.
Alieleza kuwa Niewöhner alitaka nakala hiyo ya Qur'ani kukabidhiwa watu watakaoilinda, ndiyo sababu ilipelekwa msikitini. "Nakala hii ya Qur'ani hii ya kihistoria sasa ni sehemu ya urithi wa kiroho na kiutamaduni wa jamii yetu na itabaki hapa kama urithi wa kudumu," alisema Usser. "Nakala hiyo Qur'ani itaonyeshwa katika eneo maalum la msikiti wetu, kufunguliwa kwa kila mtu kuona na kuchunguza. Kazi hii ya thamani itang'aza urithi wa kidini na kitamaduni wa jamii yetu, ikiunda uhusiano thabiti kati ya zamani na sasa na itapitishwa kwa vizazi vijavyo."
3491553