IQNA

Qiraa ya Surah al-Qadr ya Sheikh Abdul Basit

22:52 - September 28, 2020
Habari ID: 3473212
TEHRAN (IQNA)- Klipu iliyopo hapa chini ni ya qarii maarufu wa Misri Sheikh Abdul Basit Abdul Samad akisoma Surah Al Qadr ya Qur'ani Tukufu mwaka 1965 katika Msikiti Imam Hussein (AS) mjini Cairo.

Abdul Basit alizaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Almazaizah katika eneo la Armant kusini mwa Misri. Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad alikamilisha hifdhi ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10 kijijini kwake kwa Ustadh Al Amir na akahitimu aina zote za kiraa ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Abdul Basit alipewa lakabu ya 'Koo ya Dhahabu' kutokana na kiraa yake ya kuvutia na alipendwa mno na wafuatiliaji wa masuala ya Qur'ani kwa kadiri kwamba hadi sasa anatambuliwa kuwa qarii mashuhuri na anayepesndwa zaidi wa Qur'ani.

Qari huyo mashuhuri wa Misri aliaga dunia tarehe 30 Novemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

3925934

Kishikizo: abdulbasit ، qiraa ، abdul basit ، misri ، qadr ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :