IQNA

Usomaji Qur'ani Tukufu

Ustadh Abdul Basit akisoma aya za 103-104 za Sura Al-Imran

20:25 - October 28, 2022
Habari ID: 3475999
TEHRAN (IQNA)- Ifuatayo ni klipi ya zamani ya marhum Qarii maarufu wa Qur'ani Tukufu wa Misri Ustadh Abdul Basit Abdul Samad akisoma aya za 103-104 za Sura Al-Imran.

Hii hapa ni tarjuma ya aya hizo mbili.

 Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. (103)

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. (104)

captcha