
Mkusanyiko wa kila mwaka wa Ramadhani unaonyesha jukumu kuu la Qur'ani Tukufu katika maisha ya kitamaduni na kiroho ya Jamhuri ya Kiislamu, huku ukiimarisha umoja na ibada ya kidini mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu.
Hafla hiyo ilifanyika alasiri ya jana Alkhamisi katika Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran. Wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Iran na kimataifa walisoma Aya za Quran Tukufu mbele ya Kiongozi.
Hafla hii inaashiria moja ya programu muhimu za kidini ambazo kwa kawaida hufanyika mwanzoni mwa Ramadhani nchini Iran.
Mwisho wa hafla hiyo, Imam Khamenei aliwahutubia wasomaji wa Qur'ani Tukufu na kuelezea kuwa qira’a zao zilikuwa bora sana. “Kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, nawaombea nyote—wasomaji hawa na nyinyi nyote—muendelee kuwa pamoja na Qur'ani daima, na mche huu wa Qur'ani uendelee kukua siku baada ya siku. Na amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu."
Watu wa Iran, kama ilivyo kwa Waislamu katika aghalabu ya nchi duniani walianza mwezi wa funga ya Ramadhani siku ya Alhamisi, tarehe 19 Februari mwaka huu.
Ratiba za Ramadhani kote Iran zinajumuisha vikao vya kusoma Qur'ani, mipango ya hisani, na mikusanyiko ya iftar ya kijamii inayolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii.
3496481