
Taarifa zinasema, hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mashuhuri wa kidini na serikali. Sherehe hizo zilifanyika siku ya Alhamisi, Februari 19, katika mji wa Kigali, mji mkuu wa Jamhuri ya Rwanda.
Tukio hilo lilifanyika katika mfumo wa mipango ya kielimu ya kimataifa ya Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu (Muslim World League , MWL), kupitia mtandao wa taasisi na vituo vya Qur’ani, hasa katika nchi za Afrika.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Sheikh Muhammad bin Abdul Karim Al‑Issa, Katibu Mkuu wa MWL, Mufti Mkuu wa Rwanda, mawaziri kadhaa, wanazuoni wa Kiislamu na maafisa wa serikali, pamoja na idadi kubwa ya wahitimu na wapenda Qur’ani, hali inayoakisi kuongezeka kwa hadhi ya elimu ya Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu.
Katika hafla hiyo, ilisisitizwa kuwa programu za kielimu za MWL zinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali za nchi husika, kwa kuzingatia viwango vya kielimu vya kitaalamu na chini ya usimamizi wa moja kwa moja.
Aidha, wahifadhi wa Qur’ani na walimu walioteuliwa walitunukiwa, na ripoti ya kuona iliwasilishwa ikionyesha athari za kijamii na kielimu za programu hizi.
Kufanyika kwa sherehe hii mjini Kigali kunaonesha kuongezeka kwa nafasi ya Afrika katika nyanja ya shughuli za Qur’ani, pamoja na kupanuka kwa ushirikiano kati ya taasisi za Kiislamu na serikali za kitaifa, hatua iliyochangia kulea kizazi kipya cha wahifadhi wa Qur’ani na kuimarisha thamani za wastani (wasatiyyah) na mshikamano wa kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu.
Rwanda, inayojulikana rasmi kama Jamhuri ya Rwanda, ni nchi isiyo na bandari iliyoko katika eneo la Maziwa Makuu katikati ya Afrika. Uislamu uliingia nchini humo zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu, takribani asilimia 15 ya wakazi milioni 15 wa Rwanda ni Waislamu, na Rais wa nchi hiyo ameagiza kwamba Idd al‑Fitr na Idd al‑Adha zijumuishwe kama sikukuu rasmi katika kalenda ya kitaifa ya Rwanda.
4335691