iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mabalozi wa kudumu wa nchini wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika Umoja wa Mataifa wametangaza azma yao ya kuhamisisha jamii ya kimataifa iunge mkono taifa la Palestina ambalo linakabiliwa na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473899    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/11

TEHRAN (IQNA) – Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina umeungwa mkono na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri.
Habari ID: 3473631    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/08

TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia Hussein Ibrahim Taha, aliyewahi kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Chad ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa Msaudia Yousef bin Ahmad Al-Othaimeen.
Habari ID: 3473404    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/29

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa taarifa ikilaani uhalifu unaoendelea kufanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel wa kubomoa nyumba na taasisi za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473346    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/10

TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) sambamba na kulaani hatua ya kuvunjiwa heshima na kuchomwa moto nakala ya Qurani Tukufu nchini Sweden na kusema kitendo hicho kilichofanywa na wafuasi wenye misimamo iliyochupa mipaka wa mirengo ya kulia katika nchi hizo za Ulaya ni cha kichokozi na kichochezi.
Habari ID: 3473123    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/31

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ichukue hatua za dharura za kuzuia hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kunyakua ardhi zaidi Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472661    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/13

TEHRAN (IQNA) - Shirika la Ushirikkiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) limelaani vikali hujuma ya bomu ambayo ililenga msikiti huko Quetta, Pakistan na kupelekea watu kadhaa kuuawa na kujeruhiwa.
Habari ID: 3472368    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/13

TEHRAN (IQNA) –Hatua ya Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohamad kuwa mwenyeji wa kikao cha viongozi wa nchi za Kiislamu imeikasirisha Saudia Arabia na waitifaki wake.
Habari ID: 3472300    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/24

TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) umefanyika wiki hii katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Habari ID: 3472281    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/16

TEHRAN (IQNA) – Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa wito kwa kuwepo jitihada za pamoja baina ya Russia na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Habari ID: 3472241    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/29

TEHRAN (IQNA)- Kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kimefanyika Ijumaa mjini Istanbul, Uturuki kwa lengo la kujadili hatua za kuchukuliwa baada ya shambulio la kigaidi la hivi karibuni dhidi ya Waislamu waliokuwa katika Sala ya Ijumaa kwenye misikiti miwili nchini New Zealand.
Habari ID: 3471886    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/23

TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma za kigaidi zilizolenga misikiti miwili jana mjini Christchurch New Zealand na kupelekea Waislamu wasiopungua 49 kuuawa shahidi wakiwa katika Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3471878    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/16

Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA)-Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa wito kwa nchi za Kiislamu na mataifa mengine duniani kukata uhusiano wao kikamilifu na utawala haramu wa Israel na kuangalia upya uhusiano na Marekani kama njia ya kujibu sera hasimu za tawala hizo mbili dhidi ya watu wa Palestina.
Habari ID: 3471521    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/05/19

TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, OIC, Yousef bin Ahmad al-Othaimeen amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na kumshukuru kwa msimamo wake kuhusu Waislamu Warohingya na suala la uhamiaji.
Habari ID: 3471431    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/17

TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa Nne wa Idhaa za Qur'ani duniani umepangwa kufanyika mjini Cairo, Misri kuanzua Januari 28-30.
Habari ID: 3471368    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/23

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani imekuwa ikifanya "ufidhuli mkubwa" kuhusu Quds Tukufu (Jerusalem) na kuongeza kuwa njama zake hizo hazitafika popote.
Habari ID: 3471357    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/17

Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran iko tayari kushirikiana na nchi za Kiislamu bila ya masharti yoyote kwa ajili ya kuitetea Quds tukufu na kusema adui mkubwa wa Wayahudi si Waislamu wala Waarabu bali ni mradi hatari sana wa Wazayuni.
Habari ID: 3471309    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/12/14

TEHRAN (IQNA)-Kikao cha Qur'ani Tukufu na vijana Waislamu duniani kinafanyika katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran.
Habari ID: 3471239    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/31

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka serikali ya Myanmar kuheshimu haki za Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.
Habari ID: 3471102    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/08/04

TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani vikali mauaji ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo yametekelezwa na magaidi wa kundi la Kikristo la Anti-Balaka.
Habari ID: 3470982    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/05/17