IQNA

Hamas yataka OIC ichukue hatua kuzuia unayakuzi unafanya na Israel

22:28 - April 13, 2020
Habari ID: 3472661
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ichukue hatua za dharura za kuzuia hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kunyakua ardhi zaidi Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Hayo yamesisitizwa na kiongozi wa Hamas, Ismail Haniya katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Eddine El Othmani. Haniya amemtaka El Othmani afikishe ujumbe huo kwa Mfalme Muhammad XI wa Morocco ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Quds katika OIC.

Afisa huyo wa Hamas pia amesisitiza kuwa, taifa la Palestina litaendeleza mapambano yake dhidi ya Wazayuni maghasibu ikiwa ni katika jitihada za kukomboa ardhi zote za Palestina na hasa Quds Tukufu.

Wawili hao pia wamejadili hali ya sasa katika Ukanda wa Ghaza katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa hatari wa corona.

Siku ya Jumamosi, naibu mwenyekiti wa chama cha Fat'h cha Palestina Mahmoud al-Aloul alisema chama hicho kinawasiliana na madola makubwa duniani kwa lengo la kuchukuliwa hatua za kuzuia utawala ghasibu wa Israel kuendelea kunyakua zaidi ardhi za Wapalestina. Al-Aloul amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza njama hiyo ya uporaji na unyakuzi ardhi za Palestina kwa ushirikiano na Marekani katika kipindi hiki ambacho dunia inajishughulisha na janga la corona au COVID-19.

3891179

captcha