iqna

IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah:
BEIRUT (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, lengo la kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kutaka kuzusha hitilafu baina ya Waislamu na Wakristo.
Habari ID: 3477276    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/13

Kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu
GENEVA (IQNA) – Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) limepitisha azimio kuhusu chuki na ubaguzi wa kidini kufuatia tukio la uchomaji moto wa nakala ya Qur'ani nchini Uswidi lililolaaniwa vikali katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3477274    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/13

Chuki dhidi ya Uislamu
Huku Waislamu katika kona zote za dunia wakiendelea kulaani na kupinga tukio la hivi karibuni la kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Uswidi, Kitabu hicho kitukufu cha Waislamu kimechomwa moto na kutupwa nje ya Msikiti mmoja nchini Ujerumani.
Habari ID: 3477267    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/12

Katika kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Kuwait itasambaza nakala 100,000 za Qur'ani Tukufu nchini Uswidi zilizotarjumiwa kwa lugha ya Kiswidi.
Habari ID: 3477266    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/12

Chuki dhidi ya Uislamu
ISLAMABAD (IQNA) - Afisa mmoja wa Pakistani alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha sheria dhidi ya kufuru na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu zinapitishwa katika nchi zao.
Habari ID: 3477265    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/10

STOCKHOLM (IQNA) - Mamia ya Waislamu huko Uswidi wameandamana katika mji mkuu, Stockholm kulaani kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Habari ID: 3477262    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/10

Chuki dhidi ya Uislamu
ANKARA (IQNA)- Rais wa Uturuki amesema "Shambulizi la chuki dhidi ya kitabu chetu, Qur'ani, huko nchini Uswidi katika siku ya kwanza ya Sikukuu za Iddul Adh'ha, lilianika kiwango cha kutisha cha chuki dhidi ya Uislamu."
Habari ID: 3477260    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/09

Chuki dhidi ya Uislamu
ABUJA (IQNA) - Mwanaharakati wa Kiislamu wa Nigeria amelaani kitendo cha hivi karibuni cha kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi (Sweden) na kusisitiza kwamba vitendo hivyo vya kufuru vinatishia msingi wa kuishi pamoja kwa amani katika jamii.
Habari ID: 3477257    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/09

Chuki dhidi ya Uislamu
STOCKHOLM (IQNA) - Waziri wa Sheria wa Uswidi, Gunnar Strommer alisema serikali inafikiria kupiga marufuku kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu au vitabu vingine vya kidini baada ya kitendo cha kuchoma moto Qur’ani Tukufu hivi karibuni nchini humo kusababisha hasira katika Ulimwengu wa Waislamu.
Habari ID: 3477251    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/07

Chuki dhidi ya Uislamu
ISLAMABAD (IQNA) - Waislamu kote Pakistan walijitokeza mitaani Ijumaa kuandamana kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Uswdi.
Habari ID: 3477250    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/07

Chuki dhidi ya Kiislamu
DOHA (IQNA) - Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa wito wa kuwepo kwa mahubiri ya kila wiki katika misikiti kulaani kitendo cha hivi karibuni cha kuteketeza moto Qur'ani Tukufu chini Uswidi.
Habari ID: 3477245    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/06

Chuki dhidi ya Uislamu
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura kwa ombi la Pakistan kufuatia kuchomwa moto Qur'ani nje ya msikiti mmoja nchini Uswidi au Sweden.
Habari ID: 3477236    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/04

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Qur'ani Tukufu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali kitendo cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi, na kubainisha kuwa kukitukana kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu ni kuwatukana Mitume wa Mwenyezi Mungu na maandiko matakatifu.
Habari ID: 3477235    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/04

Chuki dhidi ya Uislamu
ROME (IQNA) - Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, amelaani kibali alichopewa mtu mwenye msimamo mkali kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Uswidi wiki iliyopita.
Habari ID: 3477230    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/03

Chuki dhidi ya Uislamu
STOCKHOLM (IQNA) - Serikali ya Uswidi (Sweden) Jumapili ilitoa taarifa baada ya nakala ya Qur'ani Tukufu kuchomwa moto nje ya msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo, Stockholm.
Habari ID: 3477229    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/03

Chuki dhidi ya Uislamu
MUSCAT (IQNA)- Mufti wa Oman ametoa wito wa kususiwa bidhaa za Sweden kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Uswidi (Sweden).
Habari ID: 3477228    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/02

Chuki dhidi ya Uislamu
BRUSSELS (IQNA)- Umoja wa Ulaya umelaani vikali tukio la hivi majuzi la kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya msikiti katika mji mkuu wa Stockholm nchini Uswidi, na kulitaja kuwa ni "kitendo cha wazi cha uchochezi."
Habari ID: 3477225    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/02

Chuki dhidi ya Uislamu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mataifa ya Waislamu yana wajibu na jukumu la kulaani na kupinga vitendo vya nchi za Magharibi vya kuvunja heshima matukufu ya Kiislamu, hususan Qurani Tukufu.
Habari ID: 3477223    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/01

Chuki dhidi ya Uislamu
Rais wa Pakistan Arif Alvi amelaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi (Sweden), huku akitaka kuchukuliwa hatua za kukomesha vitendo hivyo vya kufuru.
Habari ID: 3477222    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/01

Chuki dhidi ya Uislamu
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetangaza mkutano wa dharura kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu hivi karibuni katika mji mkuu wa Stockholm wa Uswidi.
Habari ID: 3477220    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/01