IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Afisa wa Pakistan asisitiza haja ya kutunga sheria za kukabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani

23:25 - July 10, 2023
Habari ID: 3477265
ISLAMABAD (IQNA) - Afisa mmoja wa Pakistani alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha sheria dhidi ya kufuru na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu zinapitishwa katika nchi zao.

Hili ni muhimu ili kuepusha mzozo wowote wa kidini katika siku zijazo, Mwakilishi Maalum wa Waziri Mkuu wa Pakistan kuhusu Maelewano ya Dini Mbalimbali na Mashariki ya Kati Hafiz Muhammad Tahir Mehmood Ashrafi alisema huko Lahore Jumapili.

Akilaani kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi chini ya mwamvuli rasmi, alisema kuwa wahusika wa matukio hayo wanataka kuleta mgongano kati ya mataifa na dini.

Ashrafi, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Pakistan,  aidha alisema kuwa magaidi waliowaua watu bila ya sababu yoyote kwa jina la Uislamu hata hawakuwa Waislamu. Alisema Waislamu wanawaheshimu manabii wote watakatifu na vitabu vya Mwenyezi  vikiwemo Biblia, Taurati na Zaburi kwani ni sehemu ya imani ya Waislamu

Alisema kuwa ni ishara nzuri kwamba dini zote zikiwemo za Kikristo, Kihindu na Sikh zililaani kuchomwa moto kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na takriban nchi zote kubwa pia zimelaani tukio hilo.

3484281

captcha