IQNA

Mazungumzo ya kidini

Uswidi: Mwandamanaji asema hakutaka kuchoma Torati

19:08 - July 16, 2023
Habari ID: 3477291
STOCKHOLM (IQNA) – Mwanamume aliyeapa kuchoma Torati na Biblia nje ya Ubalozi wa utawala haramu wa Israel katika mji mkuu wa Uswidi, Stockholm, alisema Jumamosi alichagua kutochoma moto maandiko ya kidini, vyombo vya habari vya Uswidi vimeripoti.

Licha ya kupewa ruhusa na polisi wa Stockholm kufanya maandamano ya watu watatu, mwanamume huyo alisema hakuwa na nia ya kuchoma vitabu vyovyote na badala yake akatupa njiti chini.

Sikuwahi kufikiria ningechoma vitabu vyovyote. Mimi ni Mwislamu, hatuchomi [vitabu]," Shirika la Habari la SVT limenukuku mtu huyo akiwaambia waliokusanyika kushuhudia kitendo hicho kilichokuwa kimepangwa

Ahmad A. mwenye umri wa miaka 32 alisema sababu halisi ya maandamano hayo ni kuelekeza hisia zao kuhusu fauti kati ya uhuru wa kusema na kuwaudhi wengine.

Hili ni jibu kwa watu wanaochoma Qur'ani Tukufu. "Nataka kuonyesha kwamba uhuru wa kujieleza una mipaka ambayo lazima izingatiwe," alieleza mkazi huyo wa Uswidi mwenye asili ya Syria.

“Nataka kuonyesha kwamba tunapaswa kuheshimiana, tunaishi katika jamii moja, nikichoma Torati, mwingine Biblia, mwingine Qur'ani Tukuf basi kutakuwa na  vita hapa, nilichotaka kuonyesha ni kwamba kitendo cha kuchoma moto kitabu kitakatifu si sawa,” aliongeza.

Uchomaji uliopangwa wa Torati ulitarajiwa kufanyika siku chache tu baada ya mtu mwingine kuchoma moto kurasa za Qur'ani Tukufu, kitabu kitakatifu cha Uislamu, kitendo ambacho kinaendelea kulaaniwa na Waislamu kote ulimwenguni.

Mtu ambaye aliwasilisha ombi la maandamano ya Jumamosi alisema hatua hiyo ni kujibu hatua ya kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya msikiti wa Stockholm mwezi uliopita na mhamiaji Mkristo wa Iraqi wakati wa likizo ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Nchi kadhaa za Kiislamu ziliwaita mabalozi wa Uswidi kupinga tukio hilo la uchomaji moto wa Qur'ani lililopelekea mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu yenye wanachama 57.

Siku ya Jumatano, chombo cha juu cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa kiliidhinisha kwa wingi hatua inayozitaka nchi kufanya zaidi kuzuia chuki za kidini kutokana na kuchomwa moto kwa nakala za Qur'ani Tukufu.

3484351

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi
captcha