Watetezi wa Palestina
IQNA-Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema utawala haramu wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake yoyote baada ya takriban siku 100 za vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478183 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/11
Jinai ya Israel
IQNA-Naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas ameuawa katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani ya utawala katili wa Israel katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon wa Beirut.
Habari ID: 3478137 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/03
Mapambano ya Wapalestina
IQNA - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina, Hamas, Ismail Haniya amesisitiza uthabiti na azma la harakati hiyo katika kuendeleza mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3478066 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/20
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema watu wa Palestina wataibuka katika vita dhidi ya Gaza wakiwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali.
Habari ID: 3477980 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/03
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Kuanzia jana subuhi Ijuumaa, na mara baada ya kumalizika muda wa kusimamisha vita, utawala wa Kizayuni umeendeleza mauaji ya kikatili kupindukia dhidi ya wananchi wa Ghaza huko Palestina wanaoendelea kuzingirwa kila upande.
Habari ID: 3477972 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/02
Watetezi wa Palestina
TUNIS (IQNA) - Rached Ghannouchi, mkuu wa Chama cha Ennahda cha Tunisia, alielezea Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kama zawadi kwa Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3477934 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/23
Harakati za Mapambano ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah jana Jumatano alikutana na ujumbe wa maafisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Beirut kujadili matukio ya Gaza, huku idadi ya wananchi wa Palestina waliouawa shahidi kwenye mashambulizi ya kikatili ya Israel katika eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu ikikaribia 15,000.
Habari ID: 3477931 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/23
Kimbunga cha Al Aqsa
Israel
WASHINGTON, DC (IQNA) - Asilimia 60 ya Waislamu nchini Marekani wanaunga mkono Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, dhidi ya utawala wa Israel, wakisema kundi hilo la kupigania ukombozi lilikuwa na haki katika mashambulizi yake.
Habari ID: 3477896 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/15
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na ujumbe alioandamana nao wamekutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei.
Habari ID: 3477847 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/06
Kimbunga cha Al Aqsa
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameilaani vikali Marekani kutokana na uungaji mkono wake usio na masharti kwa kampeni ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Aidha amesema utawala wa Israel umepata idhini ya Marekani ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3477842 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/05
AL-QUDS (IQNA) - Shambulio la anga la Israel limepiga msikiti mmoja huko Jenin, eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi, huku kukiwa na mashambulizi ya mabomu katika Ukanda wa Gaza ambayo yamegharimu maisha ya zaidi ya Wapalestina 4,300.
Habari ID: 3477776 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/23
TEHRAN (IQNA) - Mashambulizi ya usiku ya wanajeshi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza yamegharimu maisha ya watu 46 licha ya Hamas kuwachilia mateka wawili wa Kimarekani siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3477773 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/22
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA) Harakati ya Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imekosoa vikali kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ya kuyataka mapambano ya wapigania ukombozi Wapalestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kuwa eti ni "vurugu" na kusisitiza kwamba kinachofanyika katika ardhi za Palestina ni haki ya kujihami dhidi ya utawala unaokalia ardhi kwa mabavu.
Habari ID: 3477602 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/15
Mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya)
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa harakati za mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya) za Palestina na Lebanon wameapa kushirikiana ili kutoa jibu la pamoja dhidi ya sera za uvamizi za utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477543 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/03
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Binti mmoja wa Palestina ametekeleza operesheni ya kishujaa ya kujitoa kufa shahidi ili kujibu jinai za mtawalia za wanajeshi makatili wa Israel na walowezi wa utawala huo pandikizi.
Habari ID: 3476959 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05
TEHRAN (IQNA)- Ismail Hania na Khalid Mash'al, Mkuu wa sasa na wa zamani wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS Jumapili ya tarehe 16 Aprili waliwasili Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia wakiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa HAMAS.
Habari ID: 3476889 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/19
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kutaka kuweko harakati ya kimataifa ili kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kuhitimisha uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
Habari ID: 3476867 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)-Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, damu mashahidi wa Palestina italinda utambulisho wa Kipalestina, Kiarabu na Kiislamu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqsa ulio katika mji wa Quds au Jerusalem.
Habari ID: 3476796 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/01
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas ilionyesha upinzani dhidi ya ushiriki wa makundi ya Wapalestina katika mkutano uliopangwa kufanyika huko Sharm El-Sheikh wa Misri unaodaiwa kuwa na lengo la kupunguza hali ya wasiwasi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3476731 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/19
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel usithubutu kuhujumu na kuuvamia Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3476714 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/16