iqna

IQNA

Kiongozi wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuunga mkono Wapalestina na harakati zao za muqawama au mapambano.
Habari ID: 3474259    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/05

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema ufalme wa Bahrain kweli umeonyesha kuhusika kwake katika jinai zinazofanywa na utawala wa haramu wa Israeli dhidi ya Wapalestina kwa kumteua balozi wake wa kwanza kuhudumu katika utawala wa Israel.
Habari ID: 3474250    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/02

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesisitiza udharura wa kuendeleza mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kwa kutumia suhula na nyenzo zote.
Habari ID: 3474228    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/26

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali kikao cha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO), mawaziri na maafisa wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na viongozi wa utawala haramu wa Israel chenye lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474168    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/07

TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuni walikiuka haki za Wapalestina katika zaidi ya mara 3,800 mwezi Julai katika katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mjini al-Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474162    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/05

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameitaka Saudi Arabia iwaachilie huru mahabusu wote Wapalestina inaowashikilia na kufunga faili lao.
Habari ID: 3474161    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/05

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali uamuzi wa Umoja wa Afrika kuupa utawala haramu wa Israel hadi ya ‘mwangalizi’ katika taasisi hiyo ya nchi za Afrika.’
Habari ID: 3474122    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/24

TEHRAN (IQNA)-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imewataka wakazi wa Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan kudumisha mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuhakikisha kwamba ardhi ya Palestina inakuwa kaa la moto kwa maghasibu hao.
Habari ID: 3474092    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/11

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na harakati zingine ukombozi wa Palestina zinatafakari kuhusu kutumia nguvu kuulazimu utawala wa Kizayuni wa Israel uondoe mzingiro wake dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3474080    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/08

Taarifa ya Hamas
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza pia hayawezi kuzima harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3474069    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/04

TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina wamekutana na kusisitiza kuhusu ulazima wa kuimarisha na kudumisha umoja baina ya Wapalestina.
Habari ID: 3474057    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/30

TEHRAN (IQNA)- Viongozi wakuu wa mrengo wa muqawama wa Palestina na Lebanon wamejadili kipigo cha hivi karibuni cha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, sanjari na kubadilishana mawazo juu ya njia zinazopaswa kufuatwa ili kupata 'ushindi mutlaki' dhidi ya utawala huo haramu.
Habari ID: 3474056    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/30

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza ametoa tamko baada ya kubainika kuwa Wazayuni wanapanga kutekeleza hujuma nyingine dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds au Jerusalem.
Habari ID: 3473983    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/06

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema wananchi wa Palestina wamekaribia sana kuuvunja mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kushirikiana na Misri tokea mwaka 2007.
Habari ID: 3473968    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/01

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kufanya chokochoko na mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya mji wa Quds (Jerusalem) na Msikiti Mtukufu wa al Aqsa mjini humo.
Habari ID: 3473942    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/24

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei amejibu barua za viongozi wa harakati za mapambano ya kukomboa Palestina za Hamas na Jihad Islami akisisitiza kuwa: Nyoyo zetu ziko pamoja nanyi katika uwanja wa mapambano yenu, na hatimaye mtapata ushindi.
Habari ID: 3473941    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/24

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imetangaza ushindi katika mapambano ya siku 10 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umevamia Ukanda wa Ghaza na kuongeza kwamba waziri mkuu wa utawala huo Benjamni Netanyahu ameshindwa vibaya katika makabiliano hayo.
Habari ID: 3473928    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/20

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameutaka Umma wa Kiislamu na Kiarabu kufanya maandamano na mikutano ya kutetea na kuunga mkono Msikiti wa al Aqsa na watu wa Palestina.
Habari ID: 3473908    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/14

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amemwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumjulisha matukio na mabadiliko yanayojiri katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473894    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/10

TEHRAN (IQNA)- Kadhia ya wafungwa Wapalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni kipaumbele kwa watu wa Palestina.
Habari ID: 3473830    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/19