IQNA

Jinai za Israel

Roho zinachemka: Hamas yaonya kuhusu Isarel kuweka vizuizi vya Msikiti wa Al-Aqsa

19:21 - February 25, 2024
Habari ID: 3478412
IQNA - Kutakuwa na mlipuko na maafa makubwa hivi karibuni ikiwa utawala wa Kizayuni utaendelea na mpango wa kuwazuia Waislamu kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ilionya.

"Adui wetu ajue kwamba roho zinachemka ... hasira [yetu] imefika kiwango cha juu... na mlipuko unakuja kujibu vikwazo vyovyote vya Waislamu kuingia Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa mwezi wa Ramadhani," harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas,  ilisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Telegram siku ya Jumamosi.

Indhari hiyo imekuja siku moja baada ya ofisi ya Benjamin Netanyahu waziri mkuu katili wa utawala wa Israel kusema utawala huo utawaruhusu Waislamu kusali katika msikiti huo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaoanza Machi 10, lakini kutakuwa na vikwazo vya kuingia.

Mgogoro wa sasa katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa - ambao ulianza Oktoba 7, 2023 - kwa sehemu ulisababishwa na himya ya utawala haramu wa Israel kwa walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada ambao huuvunjia heshima mara kwa amra Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem). Harakati ya Hamas iliongoza operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa Oktoba 7 dhidi ya utawala wa Kizayuni kutokana na jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina hasa ukiukaji wa utukufu wa Msikiti wa Al Aqsa katika kipindi cha miongo saba iliyopita. Kufuatia operehseni hiyo Israel ilianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina Gaza.

Wapalestina waliona kuwa ni kunajisi sehemu moja takatifu zaidi katika Uislamu ambayo iko katika Mji Mkongwe wa Jerusalem al-Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Israel imeua karibu Wapalestina 30,000 katika Ukanda wa Gaza, wengi wakiwa ni wanawake na watoto,  tangu siku hiyo ya Oktoba.

Osama Hamdan, afisa mkuu wa Hamas, alionya Jumamosi kwamba kizuizi kilichopangwa cha sala wakati wa Mwezi  Ramadhani ni katika njama ya baraza la mawaziri la vita la Netanyahu kutekeleza hujuma kamili dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa.

Hamdan alitoa wito kwa Wapalestina wote wanaoishi katika maeneo yanayokaliwa nje ya Gaza kusimama dhidi ya mpango wa Israel wa kuwawekea vikwazo vya kusali Al Aqsa.

3487323

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al aqsa hamas israel
captcha