IQNA

kadhia ya Palestina

Hamas Kutokubali Mpango Wowote wa Kusitisha Mapigano ambao hauainishi Mwisho wa Vita dhidi ya Gaza

13:24 - June 24, 2024
Habari ID: 3479007
Afisa wa Hamas alisema pendekezo lolote la kusitisha mapigano ambalo halijumuishi kumalizika kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza litakataliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Sami Abu Zuhri alisisitiza kwamba; kusitishwa kwa vita ni sharti dhahiri la kukubali mpango wowote wa kusitisha mapigano.

 Ameonya dhidi ya kuendelea dhulma za Israel dhidi ya watu wa Palestina na kusema kuwa kunaweza kuliteketeza eneo lote kwa moto.

 Abu Zuhri pia alisema kwamba; mawasiliano na mashauriano yanaendelea kwa ajili ya kufikia usitishaji vita na kubadilishana wafungwa.

 Utawala wa Israel umekuwa ukiendesha mashambulizi ya kikatili dhidi ya Ukanda wa Gaza, yakilenga hospitali, makazi na nyumba za ibada baada ya harakati za muqawama wa Palestina kufanya mashambulizi ya kushtukiza yaliyopewa jina la Operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa, tangu tarehe 7 Oktoba, mwaka jana.

 Takriban watu 37,400 wa Ukanda wa Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa na 85,197 kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala katili wa Israel.

 Vikosi vya utawala bandia wa Israel Vilishambulia kwa Bomu Kambi ya Al Shati huku Wizara ya Afya ikiripoti vifo vya zaidi ya watu 100 kwa Siku.

N a pia, maeneo makubwa ya Ukanda wa Gaza yalikuwa magofu huku kukiwa na kizuizi cha chakula, maji safi, na dawa.

 Utawala huo bandia wa Israel unashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, (ICJ) ambayo uamuzi wake wa hivi punde uliiamuru Tel Aviv kusitisha mara moja operesheni yake huko mjini Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni 1 walitafuta hifadhi kutokana na vita kabla ya kuvamiwa Mei 6, mwaka huu.

3488855

 

 

Kishikizo: hamas israel vita
captcha