Mapambano ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya al-Umma ya Lebanon Sheikh Abdullah al-Jabri amepongeza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.
Habari ID: 3475779 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/09/13
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeulaani utawala haramu wa Israel kwa kuruhusu kuandaliwa matamasha katika Msikiti Mkuu wa Beersheba (Biʾr as-Sab).
Habari ID: 3475727 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/09/03
Harakati za Muqawama
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili.
Habari ID: 3475695 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/28
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani vikali kuendelea kupasishwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kkwa mabavu za Palestina.
Habari ID: 3475640 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/18
Mapambano dhidi ya Israel
TEHRAN (IQNA) - Afisa wa harakati ya mapambano ya Jihad Islami ya Palestina anasema mapambano na muqawama dhidi ya utawala vamizi na ghasibu wa Israel yataendelea hadi ukombozi wa ardhi zote za Palestina.
Habari ID: 3475637 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/17
Jinai za Wazayuni
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas imetoa wito wa kuundwa muungano dhidi ya vitendo vya uchokozi vya utawala wa Kizayuni wa Israel, baada ya takriban wanajeshi watatu wa Syria kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Israel dhidi ya Syria.
Habari ID: 3475627 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/15
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Jihad Islami (Jihadi ya Kiislamu) ya Palestina imelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umewaua vijana wawili Wapalestina na kusema ukatili kama huo hauwezi kuvuruga azma ya Wapalestina kupigiania ukombozi wao.
Habari ID: 3475533 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/24
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisisitiza kuhusu utambulisho wa Kiislamu wa Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuongeza kuwa, wanaosaliti Palestina kwa kuanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel wafahamu kuwa ukombozi wa Msikiti wa Al Aqsa unakaribia.
Habari ID: 3475427 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/26
Muqawama (Mapambano ya Kiislamu)
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut.
Habari ID: 3475418 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/24
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nje ya nchi amesisitiza kuwa, Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ni eneo la kidini na ni la Kiislamu kikamilifu na kwamba, wananchi wa Palestina hawataruhusu kutekelezwa njama chafu za kuliyahudisha eneo hilo takatifu.
Habari ID: 3475263 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/18
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni wameushambulia Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa mnasaba wa utawala haramu wa Israel kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Habari ID: 3475209 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/05
TEHRAN (IQNA)- Makundi mbalimbali ya mapambano ya Palestina yameitisha kikao cha dharura mjini Ghaza kutokana na utawala wa Kizayuni wa Israel kushadidisha jinai na vitisho dhidi ya wananchi wa Palestina.
Habari ID: 3475123 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/13
TEHRAN (IQNA)- Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad ya Kiislamu zimelaani vikali jinai za hivi karibuni za wanajeshi wa utawala haramu wa Israel ambao wamewaua Wapalestina akiwemo mwanamke.
Habari ID: 3475114 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/11
Matukio ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya Wazayuni wenye misimamo mikali wametoa wito wa kuhujumiwa Msitiki wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) mnamo Aprili 15 sambamba na 14 Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mnasaba wa siku kuu ya Kiyahudi wa Pasaka.
Habari ID: 3475097 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/07
TEHRAN (IQNA)- Harakati za mapambano ya Kiislamu ambazo zinapignaia ukombozi wa Palestina zimelaani vikali safari ya rais wa utawala haramu wa Israel Isaac Herzog nchini Uturuki wakati huu ambao Israel imeshadidisha hujuma dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3475026 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/03/10
TEHRAN (IQNA)- Harakati za Kiislamu za kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas na Jihad Islami zimesisitiza ulazima wa kuafikiana na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kuhusu mpango wa pamoja wa kitaifa wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikoloni ardhi za Palestina.
Habari ID: 3474978 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/26
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yamekosoa vikali kitendo cha Australia cha kuitambua harakati ya muqawama ya HAMAS kuwa ni kundi la kigaidi.
Habari ID: 3474946 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/19
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati wa Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amemtumia salamu na ujumbe maalumu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumshukuru kwa misimamo yake ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.
Habari ID: 3474932 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/15
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa onyo kali kwa utawala haramu wa Israel baada ya walowezi wake wa Kizayuni kuwashambulia tena Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474925 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/13
Ismail Haniya
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema mrengo wa muqawama au mapambano utalipiza kisasi cha damu za vijana watatu wa Kipalestina waliouawa shahidi hivi karibuni na jeshi katili la utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474916 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/11