IQNA

Vikwazo vya kiserikali vyazuia Waislamu wa Marekani kuwafikishia misaada Wapalestina Gaza

19:06 - November 30, 2024
Habari ID: 3479828
IQNA - Kuna mashirika mengi ya kutoa misaada ya Kiislamu nchini Marekani yanayojaribu kupeleka misaada Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanaokumbwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na Israel, lakini wanakabiliwa na vikwazo na ubaguzi mbalimbali.

Kitendo cha taasisi za fedha  kuweka mashirika ya Kiislamu katika orodha ya 'taasisi hatari za kufanya nazo biashara' kimekuwa na athari kubwa kwa biashara zinazomilikiwa na Waislamu na wahamiaji kwnai orodha hiyo inapelekea wakatiziwe huduma muhimu za benki.

Huku watu wa Gaza wakikabiliwa na baa la njaa na kuendelea kushambuliwa kwa nyumba zao na utawala ghasibu wa Israel, mashirika mengi ya misaada ya Kiislamu yanajaribu sana kuwasaidia Wapalestina kuwa hai na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada.

Hata hivyo, mengi ya mashirika haya yamegundua katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwamba benki wanazozitegemea kusaidia kutuma misaada hii kwa watu wa Gaza hazitaki kufanya kazi na mashirika ya misaada ambayo yanaendeshwa na Waislamu - hasa ikiwa yanakusudia kuwasaidia Wapalestina Gaza.

Amany Killawi, mwanzilishi mwenza wa LaunchGood, jukwaa la Waislamu la kutoa misaada anasema:. "Ninahisi kuna uchunguzi wa ziada juu ya mashirika ya Kiislamu."

LaunchGood ni mojawapo ya mashirika mengi ambayo yanajaribu kusaidia watu kutoka Gaza lakini sasa  akaunti zao zimefungwa bila sababu dhahiri katika mwaka uliopita. Killawi anasema anadhani benki hizi zinaogopa kutuhumiwa kuwa zinafanya kazi na mashirika ya Kiislamu wakati mjadala wenye utata juu ya mustakabali wa Israeli na Palestina ukiendelea.

Ilhan Omar, mjumbe wa chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, alikuwa sehemu ya kundi la wabunge walioomba taarifa mwezi Februari kutoka kwa benki kuu kuhusiana na kwa nini Wamarekani Waislamu wanabaguliwa. Walisema kufungwa kwa akaunti hizi kunaweza kuwa na "athari mbaya kwa wateja".

Jambo lililo wazi ni kwamba kufungwa kwa akaunti hizi si matukio ya pekee bali ni sehemu ya mwenendo mkubwa zaidi. Youssef Chouhoud, profesa msaidizi wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Christopher Newport anasema benki zimekuwa zikifunga akaunti za mashirika yasiyo ya faida yanayoendeshwa na Waislamu kwa "kiwango cha juu cha kutiliwa shaka" kwa miaka mingi.

Mambo yamekuwa mabaya zaidi huku mzozo wa Gaza ukiongezeka na mashirika kadhaa ya kibinadamu nchini Marekani na Ulaya ambayo yanajaribu kutoa chakula kwa wakazi wa Gaza yamefungwa akaunti zao za benki na shughuli kusimamishwa tangu kuanza kwa mzozo wa sasa.

Killawi anasema LaunchGood inatafuta kibali cha kusimamia malipo bila kutegemea benki kwa kutumia mfumo utakaojulikana kama  PayGood na anatumai kuwa juhudi hizi zitasaidia Waislamu kufikisha misaada Gaza na maeneo mengine.

3490871

Habari zinazohusiana
captcha