IQNA

Wanawake Waislamu Marekani wawasilisha mashtaka baada ya kuvuliwa Hijabu wakati wa maandamano

16:24 - July 02, 2025
Habari ID: 3480883
IQNA – Mwanamke wawili Waislamu nchini Marekani wamewasilisha kesi dhidi ya Kaunti ya Orange na idara yake ya sheriff, wakidai kuwa maafisa walilazimisha kuondolewa kwa hijabu zao wakati wa kuwatia mbaroni katika maandamano ya mwaka 2024 huko UC Irvine.

Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR-LA) na Shirika la Sheria la Asia (ALC), inadai kuwa Salma Nasoordeen na Shenai Aini walikumbwa na ubaguzi wa kidini wakati walipokamatwa tarehe 15 Mei 2024 katika maandamano ya kulaani jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza.

Nasoordeen anasema kuwa afisa mmoja alivua hijabu yake na hivyo kuonyesha nywele zake mbele ya kamera za vyombo vya habari.

Wanawake wote wawili wanasema baadaye waliamriwa kuondoa hijabu mbele ya maafisa wa kiume kwa ajili ya kupigwa picha za kukamatwa, jambo ambalo ni kinyume na imani zao za kidini.

“Sijawahi katika maisha yangu kuondoa hijabu kwa ajili ya picha zozote za utambulisho za serikali,” alisema Nasoordeen, kama ilivyoripotiwa na ABC7. “Kitambulisho changu, pasipoti yangu, hakuna hata kimoja. Nilijiuliza, ‘Je, inaruhusiwa? Je, ni tofauti kwa sababu nipo gerezani? Je, sina haki ya kuendelea kuvaa hijabu hapa?’”

“Nataka kuweka wazi kuwa hijabu yangu ni alama kuu ya imani yangu,” alisema Aini. “Ni utambulisho wangu, kinga yangu, na imani yangu. Mwaka mmoja baadaye, bado ninaathirika sana. Bado nasikia kilio changu cha kuendelea kufunikwa.”

Idara ya Sheriff wa Kaunti ya Orange imekanusha madai hayo, ikisema picha za kukamata hazitoiwi kwa umma na kuwa wanawake waliotakiwa kuondoa hijabu walifanya hivyo kwa faragha mbele ya maafisa wa kike tu.

Maafisa walielezea madai ya CAIR-LA kama “ya kupotosha.” Kaunti haikutaka kutoa maelezo zaidi, ikisema kesi bado iko mahakamani.

3493689

Kishikizo: hijabu marekani cair
captcha