iqna

IQNA

Watetezi wa Palestina
IQNA - Wakati wa maandamano ya wafuasi wa Palestina huko Rabat, mji mkuu wa Morocco, siku ya Jumapili, maelfu ya raia wa Morocco walitoa wito wa kukatwa uhusiano na utawala wa Kizayuni unaoendelea kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wa palestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478090    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/25

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mikutano ya hadhara imefanyika katika miji katika nchi mbalimbali za Magharibi mwishoni mwa juma kupinga mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wa palestina wa Gaza na kutaka kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa.
Habari ID: 3478086    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/24

Watetezi wa Palestina
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria chimbuko la matukio ya hivi karibuni huko Palestina na kusema kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni zinapaswa kushtakiwa kwa kufanya mauaji ya kimbari huko Gaza.
Habari ID: 3478082    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/24

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema utawala wa Israel hauwezi kufanya jinai nyingi kiasi hiki dhidi ya Wa palestina huko Ghaza bila ya uungaji mkono wa Marekani na Uingereza.
Habari ID: 3478081    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/23

Kadhia ya Palestina
IQNA-Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hatimaye limepitisha azimio kuhusu jinai za Israel dhidi ya Gaza, likidai kuongezwa kwa misaada katika eneo lililozingirwa lakini lakini limeshindwa kuulazimisha utawala haramu wa Israel usitishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wa palestina katika eneo hilo.
Habari ID: 3478078    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/23

Kadhia ya Palestina
IQNA- Chama kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha al-Wefaq kimesema hatua ya utawala wa Aal-Khalifa ya kujiunga na muungano wa baharini wa Marekani katika Bahari Nyekundu ni kusaliti kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3478077    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/23

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Kumekuwa na ongezeko mara saba la mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) nchini Uingereza kutoka Oktoba 7 hadi Desemba 13. Hayo ni kwa mujibu wa taasisi ya Tell MAMA ambayo iafuatilia matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza.
Habari ID: 3478073    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/22

Jinai za Israel
IQNA – Mji wa Al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel Ijumaa umeshuhudia vikosi vya Israel vikitumia gesi ya kutoa machozi na nguvu ziada kuwatawanya waumini karibu na eneo la Msikiti wa Al-Aqsa huku watu wengi wakiugua kwa kuvuta gesi hiyo ya machozi.
Habari ID: 3478072    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/22

Watetezi wa Palestina
IQNA - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen imetangaza kuanza mchakato wa uhamasishaji wa vijana wanaojitolea kuenda kupigana katika vita vya Gaza pamoja na wapiganaji wa harakati za Kiislamu huko Palestina.
Habari ID: 3478070    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/21

Mapambano ya Wapalestina
IQNA - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina, Hamas, Ismail Haniya amesisitiza uthabiti na azma la harakati hiyo katika kuendeleza mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3478066    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/20

IQNA Ripoti ya kutisha iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina, imefichuliwa kuwa wakati wa hujuma za hivi karibuni za kijeshi za utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, asilimia 70 ya watu 18,800 waliouawa walikuwa wanawake na watoto.
Habari ID: 3478053    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/18

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu yenye makao yake London (IHRC) amekosoa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa undumilakuwili wake linapokuja suala la kushtaki wahusika wa uhalifu wa kivita.
Habari ID: 3478050    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/17

Watetezi wa Palestina
IQNA – Toleo la 19 la Jukwaa la Kimataifa la Russia na Ulimwengu wa Kiislamu lilifanyika mjini Moscow huku wazungumzaji wakizingatia hali mbaya ya Gaza.
Habari ID: 3478028    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/13

Matukio ya Palestina
IQNA- Idara ya Habari ya Serikali ya Gaza imeripoti kwamba asilimia 61 ya nyyumba za raia wa Ki palestina huko Ukanda wa Gaza zimebomolewa katika vita vya maangamizi ya umati vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wa palestina wa eneo hilo lilolozingirwa.
Habari ID: 3478026    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/12

Watetezi wa Palestina
IQNA – Rabi au Kuhani wa Kiyahudi mwenye makazi yake nchini Marekani anasema utawala haramu wa wa Israel unatumia vibaya dini ya Kiyahudi ili kuendeleza ukatili na uvamizi wake katika ardhi za Wa palestina .
Habari ID: 3478024    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/12

Watetezi wa Palestina
IQNA - Maandamano duniani kote kupinga na kulaania mauaji ya kimbari yanayotekeleza na utawala haramu wa Israel kwa himaya ya Marekani dhidi ya Wa palestina huko Gaza yanaendelea duniani kote.
Habari ID: 3478018    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/11

Kadhia ya Palestina
IQNA - Mufti Mkuu wa Oman amewakosoa wale wanaojaribu kudhoofisha harakati za mapambano ya Kiislamu (muqawama) za Wa palestina dhidi ya jinai za utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3478014    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/09

Watetezi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)-Imamu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameashiria mpango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kutatua kadhia ya Palestina kwa njia ya kura ya maoni kwa msingi wa "kila M palestina ana kura moja", na kusema: Maneno yetu ni ya kimantiki na ya kidemokrasia.
Habari ID: 3478008    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/08

Diplomasia
MOSCOW (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kusitishwa mara moja jinai za Israel za "mauaji ya kimbari" dhidi ya Wa palestina Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478004    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/08

Watetezi wa Palestina
KARBALA (IQNA) - Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, mwakilishi wa Ayatullah Sayyed Ali al-Sistani jijini Karbala, Iraq amesisitiza uungaji mkono kwa watu wa Palestina katika kukabiliana na uchokozi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3477995    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/06