IQNA

Jinai za Israel

Inasikitisha: Binti wa miaka 6 aliyetoweka Gaza amepatikana amefariki

20:29 - February 10, 2024
Habari ID: 3478327
IQNA - Msichana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka sita, ambaye alikuwa ametoweka kwa wiki mbili baada ya gari la familia yake kufyatuliwa risasi na wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel, alipatikana amekufa.

Hind Rajab alionekana akiwa hai kwa mara ya mwisho Januari 29, wakati yeye na binamu yake Layan Hamada, 15, walikuwa pekee walionusurika katika shambulio la jeshi katili la Israel kwenye gari lao walipokuwa wakitoroka sehemu moja ya jiji la Gaza lililozingirwa.

Familia yao, akiwemo mjomba wa Hind, Bashaar Hamada, mkewe na watoto wao wengine watatu, waliuawa papo hapo.

Layan baadaye aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina (PRCS).

Miili ya Hind, Layan, na wafanyakazi wa PRCS iligunduliwa na jamaa wengine ambao walikwenda kuwatafuta katika kitongoji cha Tal al-Hawa cha jiji la Gaza.

"Hind na wengine wote kwenye gari wameuawa," babu ya msichana huyo, Baha Hamada, aliliambia shirika la habari la AFP siku ywaandishi habari Jumamosi.

Jamaa hapo awali walisema gari la familia hiyo lilikutana na vifaru vya Israel na kufyatuliwa risasi walipokuwa wakijaribu kukimbia.

Tukio hilo limezusha hasira na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu hatua za utawala wa Israel zilizopelekea vifo vya raia hao na wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu.

Tangu ilipoanza vita vyake  vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mapema Oktoba mwaka jana, watu milioni 1.9 -  yaani asilimia 85 ya wakazi wa Gaza - wamekimbia makazi yao. Mashambulizi ya Israel pia yameua takriban watu 28,000 kufikia sasa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

3487142

Habari zinazohusiana
captcha