IQNA

Jinai za Israel

Israel imeua zaidi ya raia 100 katika hujuma mpya ya mauaji ya kimbari Gaza

11:00 - February 12, 2024
Habari ID: 3478339
IQNA-Utawala katili wa Israel umeendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga na mizinga katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo na kuua na kujeruhi mamia ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, mashambulizi ya hivi punde ya kikatili ya utawala huo dhidi ya nyumba na misikiti ya watu huko Rafah hadi sasa yamesababisha vifo vya takriban raia 100 huku wengine wasiopungua 230 wakijeruhiwa. Makumi ya watu pia wamenaswa chini ya vifusi.

Afisa wa Wizara ya Afya ya Palestina alisema hospitali za Gaza haziwezi kushughulikia idadi kubwa ya majeruhi kutokana na mashambulizi ya Israel.

Mashambulizi hayo mapya yametokea baada ya vyombo vya habari vya Palestina kuripoti kuwa wanajeshi wasiopungua 11 wa Israel wameuawa katika shambulizi la kuvizia la wapiganaji wa muqawama wa Palestina karibu na mji wa Khan Yunis, pia kusini mwa Gaza.

Mashambulizi hayo pia yametokea wakati ambapo zaidi ya watu milioni moja, zaidi ya mara tano ya idadi ya watu wa kawaida wa Rafah, wamekimbilia katika mji huo huku kukiwa na mashambulizi ya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza.

Mashambulizi ya kikatili ya Israel  dhidi ya Gaza hadi sasa yamepelekea Wapalestina wasiopungua 28,000 kupoteza maisha wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwaacha wengine zaidi ya 67,700 wakijeruhiwa.

Wakati huo huo, katika kuendelea kulipiza kisasi jinai za Israel,  wapiganaji wa Wapalestina huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, wametekeleza operesheni ya kuvuzia na kuangamiza zaidi ya wanajeshi 11 wa utawala wa Israel.

3487157

Habari zinazohusiana
captcha