IQNA

Watetezi wa Palestina

Sheikh Qassem: Iran Inaunga mkono Muqawama bila kutarajia chochte mkabala

14:50 - February 03, 2024
Habari ID: 3478295
IQNA - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amepongeza uungaji mkono wa Iran kwa harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu na kusema uungaji mkono huo unafanyika bila ya kutarajia chochote mkabala wa uungaji mkono huo.

Akihutubia katika hafla iliyofanyika katika haram ya Bibi Ruqayyah (SA) nchini Syria kwa ajili ya kukumbuka Seyed Razi Mousavi, mshauri wa kijeshi wa Iran aliyeuawa shahidi na utawala wa Kizayuni, Sheikh Naim Qassem alisema Iran ni nchi huru na muungaji mkono wa muqawama.

Ameongeza kuwa Iran imetoa mkono wa urafiki kwa nchi za eneo na harakati za kupigania uhuru za kieneo ili kukabiliana na mfumo wa kibebebru na uvamizi..

Sheikh Qassem pia amesisitiza kuwa ingawa Iran inaunga mkono Hizbullah, makundi ya muqawama ya Palestina na harakati nyinginezo za muqawama katika eneo, lakini haiingilii masuala ya ndani ya nchi za eneo.

Afisa huyo wa Hizbullah pia ameashiria Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba na baadaye vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake katika hujuma hiyo ya kinyama dhidi ya kambi ya Palestina.

Alisikitishwa na ukweli kwamba baadhi wanaikosoa Hizbullah kwa kuunga mkono Gaza, akisema nchi zote za Kiislamu na Kiarabu lazima zifanye hivyo.

 “Tunawauliza: Kwa nini hawaungi mkono Gaza? Kwa nini hamsimami pamoja nao (watu wa Gaza)? Kwa nini wewe mnafuatilia kuanzisha uhusiano na Israel? Tunauliza kwa nini humuungi mkono Palestina. Ni haki yetu na haki ya Palestina, Msikiti wa Al-Aqsa na utu wa mwanadamu (kuunga mkono Palestina)."

Aliongeza: "Ni imani yetu kwamba muqawama, yaani mapambano ya Kiislamu ya taifa la Palestina yatapata ushindi."

Habari zinazohusiana
captcha