iqna

IQNA

palestina
Milad un Nabii
AL-QUDS (IQNA) - Wa palestina waliadhimisha Maulidi yaani kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) huko Al-Khalil na hasa katikak Msikiti Ibrahim huku kukiwa na vikwazo vikali vilivyowekwa na utawala haramu wa Israel ambao unaongoza kampeni ya kupinga Maulidi.
Habari ID: 3477668    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/29

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya utawala katili wa Israel siku ya Jumatano viliwashambulia Wa palestina , wakiwemo wanawake na watoto, ambao walikuwa wakiadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) huko Al Quds (Jerusalem) Mashariki. Mji huo mtakatifu unakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477664    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/28

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani uamuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi Al Quds inayokaliwa kwa mabavu (Jerusalem) na kutaka kuangaliwa upya uamuzi huo.
Habari ID: 3477647    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/24

Watetezi wa Quds Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mauritania wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott, wakilaani kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Waarabu na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3477643    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/23

Kadhia ya Palestina
AL-QUDS (IQNA) - Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa al-Quds (Jerusalem) ni mahali pa ibada kwa Waislamu peke yao na ni haki takatifu isiyopingika kwao, mkuu wa Kamati ya Juu ya Rais ya Masuala ya Kanisa huko Palestina alisema.
Habari ID: 3477628    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/20

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)-Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mauaji ya Wa palestina wa Sabra na Shatila yaliyofanywa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika ujumbe usemao: Sabra na Shatila daima litabaki kuwa doa la aibu kwenye vipaji vya waungaji mkono wa utawala wa Israel na watetezi wa kizandiki wa haki za binadamu hususan Marekani na Uingereza.
Habari ID: 3477606    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/16

Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA) Harakati ya Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imekosoa vikali kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ya kuyataka mapambano ya wapigania ukombozi Wa palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kuwa eti ni "vurugu" na kusisitiza kwamba kinachofanyika katika ardhi za Palestina ni haki ya kujihami dhidi ya utawala unaokalia ardhi kwa mabavu.
Habari ID: 3477602    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/15

AL-QUDS (IQNA) - Utawala wa Israeli umetoa idhini yake kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vipya vya walowezi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3477577    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/10

Mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya)
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa harakati za mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya) za Palestina na Lebanon wameapa kushirikiana ili kutoa jibu la pamoja dhidi ya sera za uvamizi za utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477543    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/03

Kadhia ya Palestina
Al QUDS (IQNA) - Makumi ya maelfu ya Wa palestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa ya jana iliyosaliwa kwenye Msikiti wa Al-Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) licha ya kuwekewa vizuizi na kukabiliwa na hatua kali za kiusalama zilizochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mji huo unaoukalia kwa mabavu.
Habari ID: 3477538    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/02

Watetezi wa Palestina
TUNIS (IQNA) - Rais wa Tunisia amesistiza kuwa nchi yake kati haitaanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel , akisema neno hilo halipo hata katika kamusi ya Tunisia.
Habari ID: 3477527    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/31

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - M palestina aliyekuwa na umri wa miaka 20 amefariki dunia kutokana na majeraha mwezi mmoja baada ya kupigwa risasi na askari katili wa utawala haramu wa Israel waliokuwa wakishamulia eneo moja la Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3477504    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/27

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa kilele wa BRICS ulitoa wito wa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake.
Habari ID: 3477497    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/25

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeisitiza umuhimu wa kuhifadhi hadhi ya kihistoria na kisheria ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo huko al-Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3477482    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/22

Diplomasia
ALGIERS (IQNA)- Naibu Spika wa Bunge la Algeria amesisitiza kuwa, taifa hilo la kaskazini mwa Afrika halitafuata mkumbo wa nchi nyingine za Kiarabu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, akisisitiza kuwa Waalgeria wanautazama utawala huo kuwa wa kikoloni.
Habari ID: 3477450    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/17

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wamelaani uvamizi wa mara kwa mara wa wanajeshi wa utawala haramu Israel na walowezi wa Kizayuni wenye itikadi kali kwenye jengo la Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem), na kuutaja utaratibu huo kuwa ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.
Habari ID: 3477376    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/03

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA)- Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa na vikosi vya kijeshi vya utawala haramu wa Israel vilibomoa majengo 54 yanayomilikiwa na Wa palestina huko Al-Quds (Jerusalem) Mashariki katika tarafa kubwa zaidi ya eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu mwezi Julai.
Habari ID: 3477353    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/29

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Wa palestina walishambuliwa na walowezi wa Kizayuni kwenye barabara na makutano kadhaa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Jumapili.
Habari ID: 3477299    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/18

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) – Utawala haramu wa Israel unapanga kuteka maeneo ya kiakiolojia ya Wa palestina kote Ukingo wa Magharibi, Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) ilionya.
Habari ID: 3477292    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/16

Kadhia ya Palestina
BRUSSELS (IQNA)- Katika kikao chake cha hivi karibuni kabisa, Bunge la Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa umoja huo kuitambua rasmi nchi ya Palestina.
Habari ID: 3477280    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/14