IQNA

Watetezi wa Palestina

Waislamu wa Maine wataka utawala wa Israel usitishe mauaji ya kimbari Gaza

17:44 - January 29, 2024
Habari ID: 3478273
IQNA - Mamia ya watu walikusanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Maine siku ya Jumapili kuwaandikia barua wawakilishi wao, wakiwataka kuunga mkono takwa la kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza. Wapalestina wasiopungua 26,000 wameuawa shahidi tangua utawala wa Israel uanzishe vita dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana.

Aidha waandamanaji hao wametaka  misaada ya kibinadamu ifikiswhe Gaza haraka ili kuokoa maisha ya watu akribu milioni mbili wa eneo hilo.

Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Muungano wa Palestina, ilikuwa ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina na kuishinikiza serikali ya Marekani kuchukua hatua kukomesha vita.

"Yote ni juu ya kukusanyika kama jamii kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote, kufikishwa msaada wa kibinadamu Gaza na kuweka shinikizo kwa viongozi wetu waliochaguliwa, wafanye kuunga mkono azimio la kusitisha mapigano na kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina,” alisema Brendan Davison, mratibu wa muungano huo.

Renae Al-Fdeilat, mwanajamii aliyehudhuria hafla hiyo, alisema yeye ni mke wa Mpalestina na mama wa watoto wa Kipalestina, na kwamba ana familia katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Alisema hujitahidi kuwasiliana nao kila siku kuwajulia hali.

Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa himaya ya Marekani ulianzisha  vita vya kikatili huko Gaza mnamo Oktoba 7 kufuatia operesheni ya kihistoria ya kundi la wanamapambano ya Kiislamu la Palestina, Hamas, dhidi ya utawala wa Kizayuni ambao umekuwa ukiwakandamiza wa Palestina kwa zaidi ya miongo saba.

Hadi sasa utawala katili wa Israel umeua Wapalestina wasiopungua 26,422, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine wasiopungua 65,087.

3486999

Habari zinazohusiana
captcha