iqna

IQNA

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 20 la Kongamano la Wa palestina Wanaoishi Ulaya lilifanyika Malmo, Uswidi, Jumamosi. Maelfu ya Wa palestina wanaoishi katika nchi za Ulaya walishiriki katika mkusanyiko huo, Al-Ahed News iliripoti.
Habari ID: 3477060    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/28

Muqawama
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Lebanon imesisitiza haja ya umoja na mshikamano wa kitaifa nchini humo.
Habari ID: 3477042    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/25

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) - Mufti Mkuu wa Oman aliutaka Umma wote wa Kiislamu kusimama pamoja na taifa la Palestina katika kukabiliana na uchokozi wa utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3477039    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/24

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na nchi za Kiislamu zimelaani hujuma iliyofanywa na Wazayuni wakiongozwa na mawaziri na wabunge kadhaa wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa katika kile kilichopewa jina la "siku ya bendera".
Habari ID: 3477016    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/19

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)-Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umepoteza uwezo wake na kusema: Nguvu ya kujihami ya kambi ya muqawama inapasa kuimarishwa, na muqawama wa Palestina unapaswa kuendeleza njia hiyo kwa nguvu na fahari.
Habari ID: 3476990    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/12

Uchambuzi kuhusu jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Katika mashambulizi yaliyofanywa juzi na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ambapo Wa palestina 15 waliuawa shahidi, zilichapishwa picha za uchungu huzuni za mwanamke na msichana mdogo wakiwaaga watu wa familia zao waliouliwa na jeshi la Israel, jambo ambalo limeumiza nyoyo na kuwatia watu simanzi na huzuni kubwa.
Habari ID: 3476989    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/11

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Wapigania ukombozi wa Palestina wameapa kulipiza kisasi baada ya jeshi la utawala haramu wa Israel kuwaua makamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3476981    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/09

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Mbunge mmoja wa bunge la Marekani amesisitiza upya msukumo wa kuhakikisha kwamba misaada ya nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni Israel haichangii dhuluma dhidi ya Wa palestina , hasa watoto, huku wabunge wakiendelea kutoa wito wa kuwekwa masharti kuhusu usaidizi huo.
Habari ID: 3476972    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/07

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Binti mmoja wa Palestina ametekeleza operesheni ya kishujaa ya kujitoa kufa shahidi ili kujibu jinai za mtawalia za wanajeshi makatili wa Israel na walowezi wa utawala huo pandikizi.
Habari ID: 3476959    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya kupigania ukombozi (muqawama) Palestina yameapa kuwa yatalipiza kisasi cha damu ya Sheikh Khader Adnan aliyefia shahidi ndani ya jela ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3476946    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/02

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Wizara inayoshughulikia masuala ya Wa palestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza kuwa Sheikh Khader Adnan, mfungwa M palestina amekata roho na kufa shahidi ndani ya gereza la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3476945    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/02

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema ukombozi wa Palestina na mwisho wa hali ya janga ambalo Wa palestina wanakabiliwa nalo unakaribia kwani utawala wa Kizayuni wa Israel unaonekana kuwa dhaifu kuliko hapo awali.
Habari ID: 3476928    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/28

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Kundi la kutetea haki za binadamu limeonya kuhusu njama ya utawala ghasibu wa Israel kugeuza Jumba la Sala la Bab Al-Rahma katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi.
Habari ID: 3476917    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/26

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya utawala ghasibu wa Israel siku ya Jumatatu vilimzuia mwadhini katika Msikiti wa Al-Aqsa katika jiji la Al-Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu kukamilisha.
Habari ID: 3476912    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/25

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza azma yake katika kadhia ya Palestina na kusema itaendelea kuwaunga mkono wanamapambano wa Palestina katika kukabiliana na vitendo vya kichokozi vya utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3476906    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/24

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: mkakati wa sasa wa Ulimwengu wa Kiislamu inapasa uwe ni kuwasaidia na kuwaimarisha wapigania ukombozi ndani ya Palestina.
Habari ID: 3476902    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/22

Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, haitoshi kulaani tu hujuma za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa na mashambulio dhidi ya wauminii wa Ki palestina walioko katika hali ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476894    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/20

Msikiti wa Al Aqsa
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wapatao 250,000 wa Ki palestina walishiriki katika Sala ya mwisho ya Ijumaa ya Ramadhani 2023 katika Msikiti wa Al-Aqsa jana.
Habari ID: 3476874    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/15

Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kutaka kuweko harakati ya kimataifa ili kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kuhitimisha uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
Habari ID: 3476867    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14

Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika katika kila pembe ya Iran ya Kiislamu kwa kauli mbiu kuu "Palestina mhimili wa umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu; Quds inakaribia kukombolewa".
Habari ID: 3476864    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14