IQNA

Kadhia ya Palestina

Al-Aqsa ni ya Waislamu, Kamati ya Masuala ya Kanisa la Palestina yasisitiza tena

22:38 - September 20, 2023
Habari ID: 3477628
AL-QUDS (IQNA) - Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa al-Quds (Jerusalem) ni mahali pa ibada kwa Waislamu peke yao na ni haki takatifu isiyopingika kwao, mkuu wa Kamati ya Juu ya Rais ya Masuala ya Kanisa huko Palestina alisema.

Ramzi Khoury alitoa wito kwa vyombo vinavyohusika kuongeza juhudi zao za kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa ambao "unakabiliwa na hatari iliyopo inayolenga hadhi yake ya kisheria, kihistoria na kidini," akisisitiza kwamba al-Quds "ni mji wa Palestina unaokaliwa kwa mabavu."

“Msikiti wa Al-Aqsa ni mahali pa kufanyia ibada, amani na utulivu, na unanajisiwa na watawala wanaoukalia kwa mabavu na walowezi ambao waliufanya kuwa sehemu ya dhulma na kuwakimbiza waabudu.”

Utawala vamizi wa Israel, aliendelea kusema, "umeugeuza mji unaokaliwa kwa mabavu wa al-Quds na vitongoji vyake kuwa kituo cha kijeshi ambapo Wapalestina wanafukuzwa na kuteswa."

Khoury alionya juu ya matokeo ya kudhoofisha maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo katika mji mtakatifu wa al-Quds, akisema "huu utakuwa ukiukaji wa wazi wa sheria zote za kimataifa na mikataba ya kibinadamu."

Alionya kwamba uvamizi wa walowezi katika eneo la Waislamu, na kutekeleza ibada za Kiyahudi za Talmudi  "kunaweza kuwa utangulizi udhibiti wa taratibu juu ya Msikiti wa Al-Aqsa."

Kwa hiyo, makanisa yote na waumini duniani kote lazima yalaani uchokozi unaoendelea wa Israel, alisisitiza, na pia wanapaswa kushinikiza serikali zao kukomesha "kiburi cha Israel na mpango wa kupanua mamlaka ya Kiyahudi juu ya Msikiti wa Al-Aqsa."

3485245

Habari zinazohusiana
captcha