Sayyid Abdullah al-Ghuraifi, Sheikh Muhammad Salih al-Rabiei, Sheikh Muhammad Sanqour, Sheikh Mahmoud al-Aali, na Sheikh Ali al-Sadadi walitoa taarifa ya pamoja juu ya kuwadia kwa mwezi wa Hijri wa Muharram.
Katika taarifa hiyo, wanazuoni hao wametaka kuangaziwa dhihirisho tofauti za maombolezo ya Muharram na kushiriki kikamilifu kwa makundi yote katika ibada za maombolezo.
Walisisitiza kuweka mabango na bendera nyeusi zinazoashiria kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS).
Taarifa hiyo ilisema kusawiri harakati ya Imam Hussein na kubakia na dhamira ya mafundisho yake na Seerah tukufu na waombolezaji wa Muharram ni muhimu sana.
Waombolezaji wa Ashura wanapaswa kuwa mifano ya kujitolea kwa sheria za Kiislamu na kanuni za Mwenyezi Mungu, wasomi hao walisema.
Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo katika sehemu mbali mbali za dunia hufanya sherehe kila mwaka katika mwezi wa Muharram kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.
Imamu wa tatu wa Shia Imamu Husein (AS) na kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia wake waliuawa kishahidi na kidhalimu katika zama zake - Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala katika siku ya kumi ya Muharram (ijulikanayo kama Ashura) mwaka wa 61 Hijria sawa na 680 Miladia.