iqna

IQNA

shirika la habari la qurani
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukata nyaya za vipaza sauti katika Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuzuia kuadhiniwa kwa kutumia vipaza sauti.
Habari ID: 3473816    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/15

TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Kijiji ya Utamaduni (Katara) nchini Qatar imetangaza harakati kadhaa za mitandaoni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kama vile mashindano ya Qur'ani na maonyesho.
Habari ID: 3473815    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/15

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA na vikwazo na kusema sera za Iran ziko wazi kuhusu JCPOA na vikwazo. Ameongeza kuwa sera hizo amezibainisha wazi kwa wakuu wa nchi kupitia maandishi na katika mikutano.
Habari ID: 3473814    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/14

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametuma ujumbe wa salamu za pongezi, kheri na baraka kwa Maspika wa Mabunge ya nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mfungo wa mwezi mtukuufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473812    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/14

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Misri imewaweka wanachama wengine 103 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kwenye orodha ya magaidi kufuatia hukumu zilizotolewa na mahakama za nchi hiyo.
Habari ID: 3473806    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/12

Sheikh Naim Qassim
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kuirejesha Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutakuwa ni ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3473804    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/12

TEHRAN (IQNA)-Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu yatafanyika kwa njia ya intaneti kuanzia Mei 1 hadi 10.
Habari ID: 3473801    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/11

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kimataifa Kimataifa cha Nujumu (IAC) chenye makao yake mjini Abu Dhabi kimetangaza kuwa makadirio yanayoonyesha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1442 Hijria Qamaria utaanza Aprili 13 2021.
Habari ID: 3473783    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/04

TEHRAN (IQNA)- Wanachama kadhaa wa jamii ya Qur'ani nchini Iran, wakiwemo wasomaji wakongwe wa Qur'ani, wanazuoni na wasimamizi wa taasisi za Qur'ani wamekutana Jumamosi katika ofisi za Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) katika siku ya kwanza ya kazi ya mwaka mpya wa 1400 Hijria Shamsiya
Habari ID: 3473780    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/04

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kifalme Saudi Arabia umewafuta kazi maimamu na wahubiri wapatao 1,000 katika misikiti ya nchi hiyo.
Habari ID: 3473777    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/02

TEHRAN (IQNA) – Mwakilishi wa ufalme wa Bahrain katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa amejizuia kulaani ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina
Habari ID: 3473761    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/25

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kiimla wa Saudi Arabia unapanga kuwatimua wenyeji mji wa Qatif, ambao wakaazi wake wengi ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Habari ID: 3473742    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/17

TEHRAN (IQNA)- Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemwandikia barua Ayatullah Ali Sistani kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq kumpongeza na kumshukuru kwa misimamo yake ya kuitetea na kuihami Palestina katika mkutano wake na Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.
Habari ID: 3473733    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/14

Rais Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Wazayuni na watawala wasiotaka mageuzi katika eneo wanataka vikwazo vya kidhalimu dhidi ya watu wa Iran viendelee.
Habari ID: 3473724    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/10

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Imam Baqir AS nchini Ghana kimetoa misaada ya Hospitali ya Watu Wenye Matatizo ya Kiakili ya Accra.
Habari ID: 3473720    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/09

TEHRAN (IQNA)- Fainali za Mashindano ya 37 Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ziliendelea Jumapili ambapo majaji wakiwa Tehran na maeneo mengine duniani waliwasikiliza washiriki wakisoma Qur'ani kwa njia ya intaneti. Mashindano hayo yamefanyika kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3473718    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/08

Wiki ya Maliasili na Siku ya Kupanda Miti nchini Iran
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitia kuwa, harakati za mazingira ni harakati za kidini na kimapinduzi huku akitahadharisha kuhusu uharibifu wa misitu na maliasili.
Habari ID: 3473706    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/05

Sheikh Naim Qassim
TEHRAN (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel zinajua vyema kwamba uamuzi madhubuti wa harakati hiyo wa kujibu mapigo na uchokozi wa aina yoyote hauwezi kubadilika.
Habari ID: 3473703    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/04

TEHRAN (IQNA) – Kamati andalizi ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu imetangaza majina ya jopi la majaji katika mashindano hayo.
Habari ID: 3473698    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/03

TEHRAN (IQNA) – Wiki hii kumefanyika kumbukumbu kwa mwaka mwaka wa 27 tokea Mzayuni mmoja aliyekuwa na misimamo ya kufurutu ada aliwashambulia na kuwamiminia risasi Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473688    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/28