IQNA

Israel yalaaniwa kwa kuzuia adhana katika Msikiti wa Al Aqsa

13:12 - April 15, 2021
Habari ID: 3473816
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukata nyaya za vipaza sauti katika Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuzuia kuadhiniwa kwa kutumia vipaza sauti.

Nabil Abu Rudeina, msemaji wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuzuia vitendo vya kihujuma vya utawala dhalimu wa Israel huko Palestina.

Afisa huyo wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, hatua hiyo ya Israel hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni ya kibaguzi na iliyo dhidi ya matukufu ya kidini na uhuru wa kuabudu kama ambavyo inakiuka wazi hati za kimataifa za haki za binadamu.

Kwa upande wake, Mufti wa Quds amewataka viongozi wa mataifa ya Kiarabu, ya Kiislamu na wananchi wa mataifa hayo kuchukua hatua za haraka za kusitisha hujuma za utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa.

Sheikh Muhammad Ahmad Hussein amesema katika taarifa yake kwamba, hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kukata nyaya za vipaza sauti vya Msikiti wa al-Aqsa iliyolenga kuzuia kuadhiniwa kwa kutumia vipaza sauti hiyo na kuzuia kupelekwa vifurushi vya futari kwa ajili ya wanaoswali msikiti hapo ni mwanzo wa vita vya kidini.

Mufti wa Quds amesisitiza kuwa, ulimwengu wote unabeba dhima ya hujuma na hatua hizi za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa.

Sheikh Muhammad Ahmad Hussein ametahadharisha kuhusiana na matokeo hatari kwa hatua hizo za Israel  kwa eneo zima la Asia Maghariibi kwani hatua hizo zinakinzana na dini zote za mbinguni na sheria za kimataifa.

Jumanne ya juzi iliyosadifiana na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani huko Palestina, utawala haramu wa Israel ulikata nyaya za vipaza sauti vya Msikiti wa al-Aqswa na kuzuia kuadhiniwa kutumia vipaza sauti hivyo hatua ambayo imelalamikiwa na Wapalestina.

Katika miongo ya karibuni, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umechukua hatua nyingi kwa lengo la kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa Quds tukufu, mojawapo ikiwa ni sheria ya kupiga marufuku kusomwa adhana kwa kutumia vipaza sauti katika misikiti ya mji huo.

Katika miongo ya karibuni, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umechukua hatua nyingi kwa lengo la kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa Quds tukufu, mojawapo ikiwa ni sheria ya kupiga marufuku kusomwa adhana kwa kutumia vipaza sauti katika misikiti ya mji huo.

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyahudisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

3964673

captcha