IQNA

17:52 - March 17, 2021
News ID: 3473742
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kiimla wa Saudi Arabia unapanga kuwatimua wenyeji mji wa Qatif, ambao wakaazi wake wengi ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Kwa mujibu wa sheria kitendo hicho cha kukiuka haki za wenyeji hao wa Qatif, katika mkoa wa mashariki mwa Saudia ni katika mpango wa kujaribu kukabiliana na mwamko wa wananchi wanaotetea haki zao.

Nashet Qatifi, mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Saudia , ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter Jumatatu na kufichua kuwa utawala wa kifalme nchini humo una mpango wa kutimua familia 521 za Mashia katika eneo la Qatif katika kipindi cha siku tisini. Aidha amesema mbali na kutimuliwa fmailia hizo nyumba zao pia zitateketezwa moto. Hatua hiyo imetathminiwa kuwa ni ulipizaji kisasi wa serikali baada ya wakaazi wa eneo hilo kushiriki katika mwamko dhidi ya ufalme ulioanza mwaka 2011.

Qatifi amesema familia hizo zilikuwa zimetakiwa kuuza nyumba zao na baada ya kukataa serikali imetoa fedha za kununua nyumba kwingineko lakini fedha hizo hazitoshi.

Duru katika eneo la Qatif zinasema utawala wa kifalme Saudia unmechukua hatua hiyo ili kufuta athari zozote za mwamako wa mwaka 2011 ambapo inatazmaiwa kuwa kwa kuwatawanya wakaazi, hawatakuwa tena na uwezo wa kushiriki kwa pamoja maandamano dhidi ya utawala. Aghalabu ya familia ambazo zinafurishwa ni zile ambazo zilikuwa katika mtaa wa al-Thawra (Mapinduzi) mjini Qatif.

Utawala wa Saudia umeshadidisha kamatakamata ya wapinzani wakiwemo wasomi wa Kiisalmu, waandishi na watetezi wa haki za binadamu hasa katika Mkoa wa Mashariki.

Mkoa huo umekuwa medani ya maandamano ya amani ya mara kwa mara tokea Februari mwaka 2011. Waandamanaji wanataka mabadiliko, uhuru wa kujieleza, kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa na kuhitimishwa ubaguzi wa kiuchumi na kidini dhidi ya eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa mafuta.

3474266

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: