iran - Ukurasa 9

IQNA

IQNA –Qari na Mtangazaji wa kipindi maarufu cha Qur’ani cha televisheni ya Iran, Mahfel, amesema kuwa kipindi hicho kimepata umaarufu mkubwa kimataifa, kikivutia watazamaji kutoka ulimwengu wa Kiislamu na hata katika maengine ya dunaini.
Habari ID: 3481263   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21

IQNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limewaonya maadui wa Iran hususan utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani kwamba, watakabiliwa na majibu makali na madhubuti ya Jamhuri ya Kiislamu iwapo watafanya makosa yoyote mapya au kufanya kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya nchi hii.
Habari ID: 3481262   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21

IQNA – Mwanaharakati kutoka Malaysia amesema kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuangazia mambo yanayowafungamanisha na kushikamana kukabiliana na changamoto za pamoja.
Habari ID: 3481257   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/20

Katika Kikao Nchi za Kiislamu Doha
IQNA-Katika kilele cha dharura cha nchi za Kiarabu na Kiislamu kilichofanyika jijini Doha, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, alitoa onyo kali kuhusu mashambulizi ya Israeli ya Septemba 9 dhidi ya Qatar, akisema kuwa tukio hilo linaonyesha wazi kuwa hakuna nchi ya Kiarabu au Kiislamu iliyo salama dhidi ya uchokozi wa utawala wa Tel Aviv.
Habari ID: 3481239   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/15

Mtazamo
IQNA – Shambulizi la hivi karibuni la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Qatar limethibitisha usahihi wa sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kipindi cha miaka 45 iliyopita, hususan kuhusu msimamo wa kutokufanya maridhiano na utawala wa Tel Aviv. Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Asia ya Magharibi.
Habari ID: 3481228   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/14

IQNA – Washiriki wa mkutano wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Tehran wametoa wito wa kususiwa kwa kina kwa utawala wa Kizayuni, wakilaani vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3481210   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/09

IQNA – Wanasayansi watatu mashuhuri ambao ni Mohammad K. Nazeeruddin kutoka India, Mehmet Toner kutoka Uturuki, na Vahab Mirrokni kutoka Iran wametangazwa kuwa washindi wa Tuzo ya Mustafa (SAW) ya mwaka 2025.
Habari ID: 3481206   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/09

Ayatullah Mohammad Hassan Akhtari
IQNA – Miongoni mwa malengo makuu ya shughuli na mikakati ya Wiki ya Umoja wa Kiislamu mwaka huu ni kuvuta hisia za dunia kuhusu dhulma na masaibu yanayowakumba ndugu zetu Wapalestina, afisa mmoja amesema.
Habari ID: 3481182   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/04

IQNA – Baraza la Mipango na Uratibu kutoka ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika Masuala ya Hija na Ziara, pamoja na Shirika la Hija na Ziara la Iran, wameanza maandalizi ya safari ya Hija ya mwaka ujao.
Habari ID: 3481177   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/03

IQNA-Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Iran, wakiongozwa na Ayatullah Alireza Arafi na Ayatullah Ahmad Mobaleghi, umefanya ziara ya siku tatu nchini Malaysia kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya muda mrefu ya kielimu na kidini kati ya mataifa hayo mawili.
Habari ID: 3481159   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/30

IQNA – Zaidi ya Wairani milioni tano wanasubiri kwa hamu nafasi yao ya kwenda kufanya ibada ya Umrah, afisa mmoja amesema.
Habari ID: 3481156   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/30

IQNA – Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamu yanajitahidi kuimarisha uhusiano kati ya washiriki duniani kote badala ya kuwa mashindano ya muda mfupi pekee, amebaini mtaalamu.
Habari ID: 3481148   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/28

IQNA – Hatua ya kuchagua wawakilishi wa Iran katika Mashindano ya Saba ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu imefanyika katika Shirika la Qur’ani la Wanazuoni wa Iran, Jumanne.
Habari ID: 3481141   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26

IQNA – Mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Kiislamu (OIC) ulianza Jumatatu mjini Jeddah, Saudi Arabia, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa hatua ya pamoja kusaidia Gaza na Palestina.
Habari ID: 3481136   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26

IQNA – Kikundi cha kwanza cha Wairano wanaotekeleza Umrah baada ya Hajj ya mwaka huu kimewasili Madina, Saudi Arabia baada ya kuondoka mapema Jumamosi asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini jijini Tehran.
Habari ID: 3481126   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/23

QNA – Msafara wa Qur’ani wa Arbaeen kutoka Iran, unaojulikana mwaka huu kama “Msafara wa Imam Ridha (AS)”, ulianza shughuli zake katika njia ya Arbaeen tarehe 8 Agosti 2025.
Habari ID: 3481109   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/20

IQNA – Awamu ya awali ya kategoria ya usomaji katika Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamuyaliyoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza rasmi, huku washiriki kutoka mataifa 36 wakituma video za usomaji kwa ajili ya tathmini.
Habari ID: 3481101   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/18

IQNA – Mkurugenzi wa Msafara wa Hijja wa Iran ameifu mshikamano wa kimataifa uliodhihirika wakati wa vita vya siku kumi na mbili vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ametilia mkazo umuhimu wa umoja wa Waislamu kuelekea Siku ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS).
Habari ID: 3481035   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/04

IQNA – Picha zilizopigwa mwishoni mwa Julai 2025 zinaonesha athari za mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran, mwezi Juni, ambapo maeneo ya makaazi ya raia yalilengwa.
Habari ID: 3481033   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/02

IQNA – Kundi la walimu na maqarii mashuhuri wa Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeandika barua ya wazi kwa maqari wa Misri, likiwataka wachukue msimamo dhabiti dhidi ya ukatili wa utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusimama pamoja na watu wanyonge wa eneo hilo.
Habari ID: 3481022   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30