iran - Ukurasa 5

IQNA

IQNA-Tawi la Bunge la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon limeonya kwamba, vitisho vya maneno vya Marekani dhidi ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vinaweza kushadidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3481841   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

Taarifa ya IRGC
IQNA-Shirika la Usalama la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa likisema, machafuko ambayo yamekuwa yakifanyika nchini Iran tangu mwishoni mwa Desemba yalikuwa sehemu ya "fitina iliyopangwa" na mashirika ya ujasusi ya nchi 10 maadui, kwa shabaha ya kuivuruga nchi kupitia vitendo vya vurugu, hujuma na kampeni za upotoshaji zilizoratibiwa kwa vyombo vya habari.
Habari ID: 3481839   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mpango wa maadui wa Umma wa Kiislamu ni kueneza na kuendeleza ugaidi na ukosefu wa usalama katika eneo kwa kuzusha migogoro ya ndani katika mataifa ya Kiislamu.
Habari ID: 3481838   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

IQNA – Katibu Mkuu wa Jukwaa la Kimataifa la Umoja na Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) amekutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Malaysia.
Habari ID: 3481836   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23

IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema Marekani ilichochea machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, na kwamba imefedheheka kwani njama za zimepata kipigo kikubwa cha kimkakati.
Habari ID: 3481834   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23

IQNA – Kauli za kubeza za mtawala wa Marekani Donald Trump kuhusu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zimezua lawama kali kutoka kwa Jumuiya ya Walimu wa Hawza (vyuo vya Kiislamu) katika mji mtakatifu wa Qom nchini Iran.
Habari ID: 3481829   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21

IQNA – Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Nujaba ya Iraq amesema kuwa tishio lolote dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, linachukuliwa kuwa ni tangazo la vita.
Habari ID: 3481828   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21

IQNA – Katibu Mkuu wa Jukwaa la Kimataifa la Umoja na Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu (WFPIST) amesisitiza haja ya kuimarisha umoja na kudumisha umakini wa ulimwengu wa Kiislamu kuhusu suala la Palestina.
Habari ID: 3481825   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/20

IQNA – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameisifu Iraq kwa kuwapokea mahujaji wa Kiirani wanaosafiri kuelekea nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3481819   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/19

IQNA – Jukwaa la Umoja na Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Duniani, (WFPIST) limepongeza msimamo wa kuunga mkono uliotolewa na wanazuoni na wasomi wa Kishia na Kisunni kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia machafuko ya hivi karibuni.
Habari ID: 3481814   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/18

Wizara ya Mambo ya Nje imelaani vikali tamko la hivi karibuni la kuingilia mambo ya ndani ya Iran lililotolewa na Kundi la Nchi Saba (G7), ikilishutumu kundi hilo la kiserikali linaloongozwa na Marekani kwa kuingilia masuala ya Iran na kwa mtazamo wa kinafiki kuhusu haki za binadamu.
Habari ID: 3481812   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17

IQNA-Wanazuoni na wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu, katika taarifa yao, wameonyesha kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei, kufuatia machafuko ya hivi karibuni nchini, huku wakitoa tamko linalomtaja rais Trump wa Marekani kama mtu “muhrib”
Habari ID: 3481811   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17

IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuhusika moja kwa moja Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Ulaya katika matukio ya hivi karibuni ya Iran hakukanushiki.
Habari ID: 3481809   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17

IQNA-Msikiti wa Imam Mahdi (AS) uliopo Sihat, katika Mkoa wa Mashariki wa Saudi Arabia, ulijengwa takribani miaka 132 iliyopita, na hivyo kuwa miongoni mwa nyumba kongwe za ibada katika eneo hilo.
Habari ID: 3481806   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amezionya Marekani, Israel na mamluki wao wenye mienendo ya kigaidi kama ile ya Daesh kwamba kosa lolote la kimahesabu litakabiliwa na majibu makali na ya kuangamiza.
Habari ID: 3481805   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA-Mamilioni ya watu wa Iran siku ya Jumatano wamejitokeza katika mazishi na shughuli ya kuwaaga mashahidi wa mashambulizi ya kigaidi mjini Tehran na miji mingine ya Iran.
Habari ID: 3481803   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA – Afisa na msomi mmoja wa masuala ya Qur’ani Tukufu nchini Iran amesisitiza umuhimu wa kutumia uwezo na nafasi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran yanayokuja ili kulitambulisha neno la Wahyi kwa watu wa ulimwengu.
Habari ID: 3481800   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA – Mwanazuoni wa Kiirani amesema kuwa Qur’ani Tukufu imetangaza wazi kuwa jukumu lake ni kuanzisha ustaarabu mpya, na adui analijua hilo.
Habari ID: 3481799   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA – Mamilioni ya wananchi nchini Iran waliandamana Jumatatu kulaani ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na makundi ya kigaidi yanayodaiwa kuungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3481796   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amepongeza maandamano ya kitaifa yaliyoonyesha uungaji mkono kwa Jamhuri ya Kiislamu, akisema wingi wa wananchi waliojitokeza “umeandika historia” na kuvuruga njama za maadui waliolenga kuibua misukosuko kupitia vibaraka wao wa ndani.
Habari ID: 3481795   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13