IQNA

Mkutano wa wanaharakati wa Qur'ani kutoka Khuzestan, Iran na Basra, Iraq

21:03 - May 04, 2025
Habari ID: 3480634
IQNA-Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Qur'ani ya mkoa wa Khuzestan nchini Iran na mkoa wa wa Basra nchini Iraq ulifanyika mapema wiki hii.

Wanaharakati wa Qur'ani na viongozi kutoka pande zote mbili walihudhuria mkutano huo uliofanyika katika mji wa Zubair, Basra, mnamo Alhamisi, Mei 1.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wasomi wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia na Sunni pamoja na maafisa wa Basra. Baadhi ya wanaharakati walienziwa katika hafla hiyo kwa mchango wao katika kuhudumia Qur'ani Tukufu na kuendeleza utamaduni wenye kuzingatia misingi ya Qur'ani.

Mkutano huu uliandaliwa kulingana na hati ya makubaliano (MoU) iliyosainiwa kati ya ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Khuzestan na Jumuiya ya Qur'ani ya Basra. MoU hiyo ilisainiwa mwezi Machi mwaka huu kwa lengo la kukuza uhusiano katika uga wa Qur'ani kati ya mikoa hiyo miwili na kuendeleza na kusambaza mafundisho ya Qur'ani na Ahl-ul-Bayt (AS).

Makubaliano hayo yana vipengele 12 vinavyohusiana na kufanyika kwa makongamano ya Qur'ani, kupanua shughuli za Qur'ani, kuandaa kozi mbalimbali za elimu, kubadilishana walimu na waelimishaji wa Khuzestan na Basra katika nyanja za kitamaduni, Qur'ani, sayansi na utafiti.

MoU hiyo pia inajumuisha kutuma wajumbe wa pamoja kwa ajili ya utekelezaji wa miduara ya Qur'ani katika maeneo matakatifu ya nchi hizo mbili, kubadilishana uzoefu na mafanikio ya kiutamaduni, Qur'ani na kisayansi kati ya mataifa hayo mawili, pamoja na kuendeleza uhusiano wa sekta ya Qur'ani na tamaduni za Kiislamu katika nchi nyingine kwa kuzingatia Qur'ani na Ahl-ul-Bayt (AS).

3492916

captcha