IQNA

Ayatullah Khatami

'Magaidi wa Daesh wanatumiwa na Marekani kuvuruga amani ''

19:08 - June 27, 2014
Habari ID: 1422882
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema, 'kundi la kigaidi la Daesh ni silaha mpya ya Marekani na madola mengine ya kibeberu inayotumiwa kwa lengo la kuvuruga usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

Ayatullah Ahmad Khatami ameashiria matukio ya eneo pamoja na jinai za kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq na kusema kwamba, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni zinaunga mkono kifedha na kisilaha kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq ambalo linaendesha jinai zake kwa jina la Uislamu lengo likiwa ni kuchafua sura ya Uislamu duniani.
Ayatullah Khatami ameendelea kusema kuwa: "Marekani, Uingereza, Utawala wa Kizayuni na vibaraka wao katika eneo ndio waliopanga machafuko ya sasa Iraq ili waweze kuigawa nchi hiyo vipande vipande na kwa njia hiyo wadhamini usalama wa utawala wa Kizayuni katika eneo." Khatibu wa Sala ya Ijumaa amesema kile kinachojiri sasa Iraq si vita vya Masuni na Mashia na kwamba kundi la Daesh halina utambulisho wa kidini hata kidogo na kwamba chimbuko lake ni chama cha Baath kilichotenda jinai wakati Iraq ilipokuwa ikitawaliwa na  dikteta Saddam Hussein aliyenyongwa.
Ayatullah Khatami amesema maulamaa na wanazuoni wa Kishia na Kisunni Iraq wametangaza bayana kupinga makundi ya kitakfiri na kigaidi kama Daesh. Amesema magaidi watenda jinai wa Daesh wanawaua Masuni na Mashia na hata wameshawaua maulamaa wa Kisunni ambao hawakuwa tayari kushirikiana nao katika vitendo vya kigaidi. Khatibu wa Sala ya Ijumaa pia ameashiria kimya cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mbele ya ugaidi wa Daesh huko Iraq na kusema baraza hilo limeshindwa kuchukua hatua zozotoe kwa sababu kinara wake ni Marekani na hiyo ni ishara tosha kuwa madola ya Magharibi yanasema uongo wakati yanapodai kwamba yanapambana dhidi ya ugaidi. Amesema hatimye wananchi wa Iraq kwa umoja wao wataweza kuvunja njama za magaidi nchini humo. Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Khatami amesema madola ya kibeberu yamebainisha wazi uadui wao dhidi ya Uislamu. Amesema uhasama wao dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran ni mfano wa uadui dhidi ya Uislamu kwani madai yasiyo na msingi kuwa eti Iran inataka kuunda bomu la nyuklia ni kisingizio tu cha kuiandamana Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu iko katika eneo la kistratijia la Mashariki ya Kati na imeanzisha mfumo wa utawala wenye kuzingatia mafundisho halisi ya Mtume Muhammad SAW.

1422861

captcha