Sayyid Nasrullah amesema hayo katika mazungumzo yake na Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran mjini Beirut. Nasrullah pia ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono mapambano siku zote.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameisifu harakati ya Hizbullah kwa kupambana na makundi ya kigaidi na kitakfiri na kusema kuwa, stratejia zake zimepelekea iwe na nafasi na kupata mafanikio zaidi. Shamkhani ameongeza kuwa, Harakati ya Hizbullah ina nafasi muhimu katika kuleta uwiano wa kisiasa na kiusalama nchini Lebanon.
Wakati huo huo Ali Shamkhani amesema kuwa Iran itaendeleza kwa dhati msimamo wake mkuu wa kuiunga mkono kikamilifu nchi rafiki na ndugu ya Syria, ambayo iko mstari wa mbele kupambana na ugaidi.
Shamkhani ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais Bashar al Assad wa Syria hapo jana huko Damascus. Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran pia ameisifu serikali ya Syria na wananchi wa nchi hiyo kwa kuonyesh muqawama usio na kifani dhidi ya magaidi wa kitakfiri wa Daesh na kusisitiza kuwa uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Syria kwa Rais Bashar al Assad umekuwa msingi wa mafanikio ya jeshi la Syria katika kuikomboa miji ya kistratejia iliyokuwa ikishikiliwa na wanamgambo wa Daesh.../mh 1456011