IQNA

Erdogan: Waislamu ndio waliovumbua Amerika

16:41 - November 17, 2014
Habari ID: 1474359
Rais Rajab Tayyib Erdogan amesema Bara Amerika lilivumbuliwa na Waislamu katika karne ya 12 Miladia, karibu karne tatu kabla ya Christopher Columbus kufika hapo.

“Uhusiano wa Amerika ya Latini na Uislamu ulianza karne ya 12 Miladia, Waislamu walivumbua Bara Amerika mwaka 1178, na si Christopher Columbus,” alisema Erdogan  alipohutubu katika kongamano la kimatiafa la viongozi Waislamu kutoka Amerika ya Latini.
“Mabaharia Waislamu waliwasili Amerika mwaka 1178. Columbus mwenyewe alitaja kuwepo msikiti katika mlima ulio katika Pwani ya Cuba,” alisema Erdogan.
Ameongeza kuwa Uturuki iko tayari kujenga upya msikiti katika eneo hilo.
Vitabu vingi vya historia vinadai kuwa Columbus ndie aliyekuwa mtu wa kwanza wa kigeni kufika bara Amerika mwaka 1492 wakati akitafuta njia mpya ya baharini kuelekea India.../mh

1473833

Kishikizo: erdogan cuba uturuki
captcha