IQNA

Rais wa Cuba alaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel Gaza ni fedheha kubwa

10:30 - December 28, 2023
Habari ID: 3478104
IQNA-Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba amelaani vikali mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kueleza kwamba, mauaji hayo ya kimbari ni kashfa na fedheha kwa ubinadamu.

Rais wa Cuba amesisitiza kuwa, nchi yake daima itaendelea kuunga mkono na kutetea haki za taifa la Palestina.

Rais wa Cuba amesema katika ujumbe wake wa aliaondioka katika mtandao wa kijamii wa X kwamba, kinga ya Israel ya kufanya mauuaji dhidi ya Wapalestina itaendelea mpaka lini? Mauaji haya yataendelea kufanyika kwa uhuru kamili mpaka lini?

Rais wa Cuba amesisitiza kuwa, hakuna wakati ambao nchi yake ilipuuza yale yanayojiri huko Palestina na katu haitafanya hivyo na daima imekuwa ikipaza sauti ya kuunga mkono wananchi wa Palestina.

Kabla ya hapo na katika kujibu jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, Rais wa Cuba aliitaja Marekani kuwa mshirika wa kihistoria wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kwamba, historia haitowasamehe watu wasiojali na wenye kupuuza mambo.

Kadhalika Rais huyo wa Cuba amesema kuwa, ni wakati wa kukomesha falsafa ya uporaji ili falsafa ya vita ife.

Wakati huo huo, makumi ya wananchi wa Cuba wameandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Havana na kulaani mauuaji ya kizxazi yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

3486584

Habari zinazohusiana
captcha