Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, Jumanne alikosoa vikali jarida la vichekesho lililochapisha picha hiyo, akisema kitendo hicho ni “uchochezi mchafu”.
Maandamano yalipoibuka mjini Istanbul, mhariri mkuu wa jarida hilo alisema picha hiyo ilieleweka vibaya na haikuwa “na lengo la kumvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW)”.
“Hatuwezi kumruhusu mtu yeyote kuzungumza vibaya kuhusu maadili yetu matakatifu, bila kujali hali,” alisema Erdogan katika maelezo yake yaliyoonyeshwa kwenye televisheni.
“Wale wanaomuudhi Mtume wetu na manabii wengine watachukuliwa hatua za kisheria,” akaongeza.
Erdogan alisema mamlaka zilishika nakala zote za jarida lililotolewa na wanalichunguza kwa uangalifu suala hilo kisheria.
Maelezo ya rais yalizidisha mwitikio mkali wa lawama rasmi siku moja baada ya wachora picha wanne wa jarida la LeMan kukamatwa kwa picha hiyo.
Katuni hiyo iliyochapishwa siku chache baada ya mashambulizi ya Israeli dhidi ya Iran ya siku 12, ilielezwa kuwa inaonyesha Mtume Muhammad (SAW) na Mtume Musa (AS) wakinyakuwa mikono angani juu ya mandhari ya vita.
Kibonzo hicho kilizomewa pia na viongozi wa kidini, huku jarida likiomba radhi kwa wasomaji walihisi kuudhiwa na kusema picha hiyo ilieleweka vibaya.
Mhariri mkuu wa jarida, Tuncay Akgun, aliiambia AFP kwa simu kutoka Paris kuwa picha hiyo ilieleweka vibaya.
Picha hiyo “haina uhusiano wowote na Mtume Muhammad (SAW),” alisema Akgun na kuongeza, “Sisi hatutawahi kuchukua hatari kama hiyo.”
Zaidi ya watu 200 walikusanyika kuandamana dhidi ya LeMan katikati ya Istanbul Jumanne, licha ya marufuku ya mikusanyiko na uwepo mkubwa wa polisi.
3493680