Ayatullah Qassim ameashiria malalamiko ya amani ya wananchi wa Bahrain na kusisitiza juu ya kuendelezwa malalamiko ya amani ya wananchi dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Kiongozi huyo wa kidini ambaye amekuwa akiandamwa na utawala wa Manama kwa mara nyingine tena amezikosoa siasa na sera za utawala wa Baharin na kusisitiza juu ya kudumishwa harakati ya kutaka mageuzi nchini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, maelfu ya Wabahraini jana walifanya maandamano makubwa kumuunga mkono Ayatullah Sheikh Issa Qassim, ambaye amekuwa akiandamwa mara kwa mara na maafisa wa utawala wa kidikteta wa Aal-Khalifa. Maandamano hayo mbali na kulaani utawala wa nchi hiyo, washiriki wake walilaani pia vitendo vya kushambuliwa shakhsia wa kisiasa na kidini na kusisitiza kuwa, kamwe hawatonyamazia kimya vitendo hivyo.../mh