Kitakuwa kituo cha tano rasmi cha kufundisha Qur'ani kilichoanzishwa kama sehemu ya mradi wa wa Risalatallah.
Kituo cha Kimataifa cha Qu'rani na Uenezi cha Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) kinatekeleza mradi wa Risalatallah kwa lengo la kuinua uwezo wa Qur'ani wa Iran katika ngazi ya kimataifa.
Hujjatul Islam Hosseini Neyshabouri, Mkuu wa Kituo cha Kituo cha Kimataifa cha Qu'rani na Uenezi cha ICRO amesema Akademia ya Qur'ani ya Dar An-Nur itatoa mafunzo kwa wanafunzi hapo Dar na kusaidia kuimarisha vituo vya mafunzo ya Qur'ani vya mkoa huo.
Amesema academia hiyo itaandaakozi na programu mbalimbali za ana kwa ana na za mtandaoni katika nyanja kama vile qiraa, kuhifadhi, kutafakari maana ya aya za Qur'ani n.k.
Aidha amesema Qur’ani Tukufu imeteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu kwenye wokovu na ukamilifu.
Kwa utekelezwaji sahihi wa mafundisho ya Qur'ani, machafuko yanayozikumba jamii za wanadamu yataondolewa na haki itatawala duniani, alisema.
Hujjatul Islam Hosseini Neyshabouri amebainisha kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei amesisitiza hadhi maalumu ya Qur'ani Tukufu na jinsi jamii za Kiislamu duniani zinavyoweza kupata maendeleo ya kiroho na kimaada kwa kufuata mafundisho ya Kitabu hicho Kitukufu.
Ndio maana kufundisha Qur'ani na kuitangaza ni muhimu sana na kuanzisha vituo vya Dar-ul-Quran katika nchi mbalimbali kunaweza kuwa hatua madhubuti ya kueneza mafundisho ya Qur'ani, amebaini.
4251185