Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa James W. Rawley amesema kuwa kuvunja nyumba kama njia ya kuwaadhibu Wapalestina kunakinzana na sheria za kimataifa na kunapaswa kusitishwa mara moja. Rawley amesema kuharibu nyumba za Wapalestina ni adhabu ya umati inayotumiwa kuwaadhibu watu kwa vitendo ambavyo hawakufanya. Amesisitiza kuwa vitendo hivyo vya utawala ghasibu wa Israel vina taathira mbaya sana hususan kwa watoto wadogo, wanawake na watu wazima.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitumia mbinu ya kuvunja nyumba za raia wa Palestina katika ameneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ukidai kwamba baadhi ya Wapalestina hao wanashiriki katika vitendo vya kuwahujumu askari wake.../mh