Akihutubia katika msikiti wa al-Aqswa huko Palestina, Iyad Amin Madani amesisitiza kuwa, kuingia na kuswali katika msikiti huo mtakatifu ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu ni haki ya Waislamu wote ulimwenguni.
Katibu Mkuu wa OIC amesema bayana kwamba, lengo la utawala wa Kizayuni wa Israel la kuwazuia Waislamu na kuwawekea vizingiti vya kuingia katika Masjdul Aqswa ni mwenendelezo wa uvamizi na hujuma za Wazayuni dhidi ya msikiti huo mtakatifu na wenye historia kongwe.
Wakati huo huo, Adnan al-Husseini, Waziri wa Masuala ya Quds katika serikali ya Palestina ametangaza kuwa, msikiti wa al-Aqswa na Quds ni maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa mno na nchi za Kiislamu na Kiarabu.../mh