Netanyahu amechukua hatua hiyo baada ya gazeti la Uingereza la Daily Mail kutoa ripoti iliyodai kuwa, Umoja wa Ulaya ndio uliofadhili ujenzi wa nyumba hizo za Wapalestina. Utawala wa Kizayuni wa Israel umedai kuwa Umoja wa Ulaya kwanza ulipasa kuomba kibali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Msemaji wa umoja wa Ulaya jana alitetea hatua ya umoja huo ya kufadhili ujenzi wa nyumba hizo mpya za raia wa Palestina. Shadi Othman afisa mawasiliano katika ofisi ya Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza juzi aliliambia gazeti la Daily Mail kuwa, mradi huo ni sehemu ya kazi iliyotekelezwa kwa minajili ya kuandaa mustakbali wa nchi ya Palestina. Othman ameongeza kuwa, Wapalestina wana haki ya kuishi huko, kujenga shule na kuwa na maendeleo ya kiuchumi.../mh