IQNA

Barua ya Kiongozi Muadhamu yafasiriwa kwa lugha 21

16:56 - February 28, 2015
Habari ID: 2910931
Shirika la Mawasiliano na Utamaduni wa Kiislamu Iran (ICRO) limetayarisha tarjama ya Barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa lugha 21 duniani.

Idara ya masuala ya kimataifa ICRO imetoa taarifa na kusema  hatua hiyo inalenga kukabiliana na njama zozote za kupotosha ujumbe muhimu wa barua hiyo.
Barua hiyo imetarjumiwa lwa lugha kama vile Kurusi, Kikroatia, Kiserbia, Kubulgaria, Kiswahili, Kuturiki, Kiindonesia, Kichina, Kijapani, Kihispania, Kithailand na Kialbani.
Barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini ambayo imeendelea kuakisiwa katika pembe mbalimbali duniani ina nukta kadhaa muhimu. Nukta ya kwanza muhimu ni kutolewa ujumbe huo wa Januari 21  katika kipindi hiki cha kuongezeka mashambulio na hujuma za maadui wa Uislamu na njama zao za kutaka kuuchafua Uislamu na kuonesha kwamba, dini hii ni dini ya utumiaji mabavu.
Nukta ya pili muhimu katika ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni wito wake kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini wa kuwataka wafanye uchunguzi wao wenyewe bila ya kupitia kwa mtu kuhusiana na dini ya Kiislamu.

Wachambuzi wa masuala ya Kiislamu wameutaja ujumbe huo kuwa ni wa kihistoria na wa aina yake. Nukta nyingine ya tatu muhimu katika barua hiyo ya Ayatullahil Udhma kwa vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini ni pale alipoashiria  kwamba, kuna njama nyingi zimefanyika katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyopita, takriban tangu baada ya kusambaratika Umoja wa Kisovieti kwa ajili ya kuifanya dini tukufu ya Kiislamu kuwa adui mkubwa anayetisha.
Katika sehemu moja ya ujumbe huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema “Nyote mnajua vyema kwamba, kujaribu kuidunisha na kueneza chuki na woga dhidi ya wengine ndiyo mbinu kuu inayotumiwa na watu madhalimu wanaopenda kujinufaisha binafsi. Natumia fursa hii kukutakeni mjiulize ndani ya nafsi zenu kwamba kwa nini siasa kongwe za kueneza woga na chuki, hivi sasa zimeongezewa nguvu mno kwa namna isiyo na mfano dhidi ya Uislamu na dhidi ya Waislamu? Kwa nini muundo wa nguvu duniani hivi sasa unapenda kuiweka pembeni fikra ya Kiislamu na kuwa mkali kila fikra hiyo inapojitokeza? Kwani kuna kitu gani kizuri na cha thamani ndani ya Uislamu ambacho kinasumbua mipango ya madola makubwa na hivi kuna manufaa gani yanayopata madola hayo pale yanapoeneza sura ghalati na isiyo sahihi kuhusu Uislamu? Hivyo basi ombi langu la kwanza kabisa kwenu ni kufanya uchunguzi na udadisi kuhusu misukumo na malengo ya kufanyika kampeni kubwa mno ya kuenezwa sura isiyo sahihi kuhusiana na Uislamu.”.../mh

 

2896067

captcha