IQNA

Magaidi wa Boko Haram wanaiga wenzao wa Daesh (ISIL)

14:10 - March 05, 2015
Habari ID: 2930964
Kundi la wanamgambo wa kitakfiri la Boko Haram lenye makao yake nchini Nigeria hivi sasa linaiga mbinu sawa na zile zinazotumiwa na kundi la kigaidi na kitakifiri la Daesh (ISIL) nchini Syria.

Mwishoni mwa wiki lilivishambulia visiwa vitatu huko Niger na kuua watu 19. Al Haji Aboubacar aliyetajwa kuwa ni mbunge kutoka katika mji wa Bosso kusini mashariki mwa Niger amesema kuwa wamepokea taarifa za kuuliwa watu wasiopungua 19, ambao wengi waliuliwa na Boko Haram imma kwa kuchomwa moto wakiwa hai au kuzamishwa ndani ya ziwa. Afisa huyo ameongeza kuwa watu waliozamishwa ndani ya ziwa katika hujuma hiyo iliyofanywa na Boko Haram tarehe Mosi mwezi huu wengi walikuwa ni wanawake na watoto, ambao walikuwa wakikimbia machafuko kwa kusafiri wakitumia mtumbwi ambao hata hivyo ulipinduka katika ziwa Chad, kwenye mpaka wa pamoja wa Cameroon, Nigeria, Niger na Chad. Mbunge huyo kutoka katika mji wa Bosso wa huko Niger ameongeza kuwa, watu wawili pia walijeruhiwa vibaya kwa risasi na Boko Haram. Wanamgambo wa Boko Haram kwanza waliwafyatulia risasi watu, kupora maduka na kuzichoma moto nyumba kabla ya kuvishambulia visiwa hivyo viwili.../mh

2925657

captcha