IQNA

Daesh (ISIL) wabomoa misikiti zaidi mjini Mosul, Iraq

5:33 - March 08, 2015
Habari ID: 2944654
Kundi la kigaidi na kitakfiri linalojiita Daesh (ISIL) limebomoa msikiti mwingine wa kihistoria katika mji wa Mosul nchini Iraq.

Msikiti wa Hamou al-Qadu ulibomolewa kikamilivu na magaidi wa Daesh ambao wamebomoa makumi ya misikiti na maeneo mengine ya kidini katika mkoa wa Nainawah nchini Iraq. Msikiti uliobomolewa ulijengwa mwaka wa 1880 Miladia katika zama za utawala wa Othmaniya. Mwezi uliopita pia magaidi hao wa Kiwahabi walibomoa msikiti wa kale zaidi katika mkoa wa Al Anbar nchini Iraq. Kundi la kigaidi la Daesh (ISIL, ISIS au IS) linadhibiti baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq. Kundi hilo lilianzisha kampeni ya ukatili nchini Iraq mnamo Juni 2014 wakati magaidi wa kundi hilo walipovamia na kuuteka mji wa Mosul. Magaidi hao wametekeleza jinai za kinyama dhidi ya Masunni, Mashia, Wakurdi na Wakristo katika maeneo hayo. Serikali ya Iraq inazituhumu baadhi ya nchi jirani kuwa ndizo zinazounga mkono kundi la Daesh. Serikali ya Syria imeitaja Marekani na waitifake wake katika eneo yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Saudi Arabia, Qatar na Uturuki kuwa ndio waungaji mkono asili wa magaidi wa Daesh.../mh

2938217

 

captcha