IQNA

Saudia yadondosha mabomu katika Masjid Imam Hadi AS huko Sa'ada Yemen

19:42 - May 09, 2015
Habari ID: 3276823
Ndege za kivita za Saudi Arabia zimeendelea hujuma zake za kikatili nchini Yemen na mara hii zimehujumu kwa mabomu msikiti wa kihistoria ujulikanao kama Masjid Imam Hadi AS katika mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Mayadeen ndege za Saudia zimetekeza hujuma ya kinyama dhidi ya mkoa huo wa Yemen ambapo mbali na kuhujumiwa misikiti, mahospitali na shule idadi kubwa ya raia wakiwemo wanawake na watoto wameuawa shahidi.
Licha ya Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia kudai kuwa nchi hiyo ina mpango wa kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Yemen kwa muda wa siku tano, lakini bado ndege za kivita za utawala wa Aal Saud zimeendeleza jinai zake kwa kuyashambulia maeneo tofauti ya taifa hilo. Ndege za kivita za Saudia, jana usiku ziliyashambulia maeneo kadhaa ya mkoa wa Sa’da, kaskazini mwa Yemen. Mbali na mashambulizi ya anga, maeneo kadhaa ya mkoa huo yalikuwa shabaha ya hujuma za mizinga ya jeshi la Saudia. Hii ni katika hali ambayo ndege za kivita za utawala huo zilifanya hujuma nne dhidi ya uwanja wa ndege wa Itq katika mkoa wa Shabwa, kusini mwa Yemen, na kuulenga pia kwa makombora uwanja wa ndege wa Sana'a. Kama ilivyokuwa kwa ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel katika kushambulia makaburi huko Ukanda wa Gaza, hapo jana pia ndege za utawala wa Aal Saud, zililishambulia kaburi la Sayyid Hussein Badrud-Din al-Huthi, Mwasisi wa Harakati ya Answarullah ya Yemen huko mkoani Sa’da na kusababisha hasara kubwa. Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu wa Kamati ya Maulama wa Kiislamu nchini Yemen,  Sheikh Abdus Salaam al Wajih, amelaani hujuma hizo na kusema kuwa, kushambulia kaburi la mwanachuoni huyo, hakuwezi kufuta hata kidogo fikra yake kwa Wayemen bali kutapelekea raia wengi wa taifa hilo kuzidi kumuenzi. Maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ma'ribhayakusalimika pia na mashambulio hayo ya kikatili, ambapo watu kadhaa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Kwa upande wake, khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa jana mjini Sana'a amesisitiza juu ya udharura wa kusitishwa mashambulizi hayo ya kinyama, na kusema kuwa hakuna nchi yenye haki ya kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo la Kiarabu na kwamba, makundi mbalimbali ya Wayemen yatataua matatizo yao ya ndani wao wenyewe kupitia mazungumzo baina yao. Akiashiria kuuawa na kujeruhiwa maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo, khatibu huyo wa sala ya Ijumaa ya Sana’a amesema kuwa, katika hali ambayo maadui wanafanya jinai kubwa dhidi ya binaadamu, kwa upande mwingine wanaficha maovu yao kwa kujifanya kutoa misaada kwa raia wa Yemen. Hii ni katika hali ambayo tume ya kuchunguza hasara zitokanazo na mashambulizi hayo, imetangaza kuwa zaidi ya watu 2,000 wamekwishauawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa. Mbali na hapo Kamati ya maulama nchini Yemen, kupitia Katibu wake Mkuu imeitaka Saudia kusitisha mashambulizi yake ya kinyama nchini mwao bila ya masharti yoyote. Hii ni katika hali ambayo, licha ya Saudia na waitifaki wake kama vile Marekani, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi kadhaa za Kiarabu kuendeleza mashambulizi yao na kuharibu miundombinu ya taifa hilo, lakini zimeshindwa kufikia malengo yao ya kulipigisha magoti taifa la Yemen.../mh

3276783

captcha