IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah

Iran imetusaidia kuwashinda Wazayuni

13:50 - May 25, 2015
Habari ID: 3307601
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria kwa kuuunga mkono muqawama katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sayyid Hassan Nasrullah alisema hayo jana usiku (Jumapili) katika hotuba aliyoitoa kwenye sherehe maalumu za muqawama na ukombozi wa kusini mwa Lebanon na kuitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria kuwa marafiki wenye ikhlasi wa muqawama kama ambavyo amewashukuru wote waliochangia ushindi wa harakati ya muqawama huko Lebanon.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni ulishindwa vibaya na kulazimika kukimbia kwa madhila kusini mwa Lebanon mwaka 2000 na kwa hakika huo ulikuwa ni ushindi wa aina yake kwa Lebanon.

Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulikimbia wenyewe bila ya kuweka masharti yoyote baada ya kuzidiwa nguvu na wanamapambano wa Kiislamu wa Lebanon.../mh

3307391

captcha